MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa boti ya MV Bulombora iliyofanyiwa matengenezo makubwa na kikosi cha 821 KJ Bulombora hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
Na Alex Sonna-KIGOMA
MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena amezindua boti ya MV Bulombora na kuwa itakua chachu ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa jeshi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini, Brigedia Jenerali Mabena amesema hatua ya kulifanyia matengenezo makubwa bodi hilo ni katika kutekeleza mpango wa JKT wa kuongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo na uvuvi.
“Kupitia mpango mkakati wa kujitosheleza kwa chakula kwa JKT umesukuma kufanyia matengenezo boti hii na hata baada ya Mkuu wa JKT kuridhia mradi huo baada ya kuona utakuwa na manufaa kwa jeshi na nchi kwa ujumla,” amesema.
Amesema mbali na boti hilo kutumika katika shughuli za uvuvi, lakini pia kitatumia katika kuimalisha ulinzi katika Ziwa Tanganyika, kupambana na uvuvi haramu na uhalifu wa aina zote.
“Kikosi cha 821 Kikosi cha Jeshi Bulombora mkao wake kiko pembezoni mwa Ziwa Tanganyika na kwenye ziwa kuna fursa nyingi za usafirishaji, shughuli za uvuvi kutokana na kuwapo kwa aina mbalimbali za samaki.”
Amesema boti hiyo inauwezo wa kubeba abiria kati ya watu 30 mpaka 60 na uwezo wa kubeba mzigo kati ya tani 60 mpaka 80 kwa wakati mmoja.
"Unaona kwa jinsi ambavyo inaenda kupunguza tatizo la usafiri na mwisho wa siku itakapokuwa kwenye operation itatoa ajira kwa wana Kigoma,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
Amesema boti hiyo imefanyakazi vizuri tangu mwaka 1984 ambapo ilipofika 2004 ikawa imechakaa ila kwa sasa ipo katika muonekano mpya na kwenye ubora.
"Kwa kweli ilikuwa inakatisha tamaa lakini, kwa sasa ipo katika muonekano mzuri niwapongeze makamanda wote wa vikosi," amesema Brigedia Jenerali Mabena.
Brigedia Jenerali Mabena amiwataka viongozi wa kikosi hicho kuhakikisha wanakitunza chombo hicho ili kidumu kwa muda mrefu.
"Naweka msisitizo, zingatieni kufanya service (matengenezo), muda wa matengenezo ukifika fanyeni, kama ni kumwaga oil basi ni vyema ikamwagwa kwa wakati unaotakiwa kama kuna namna ya kubadilisha kitu chochote tubadilishe kwa wakati kwa kufanya hivyo chombo hicho kitadumu na kitafikisha miaka 50,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
"Sisi tutafanya kama timu na walichokifanya hawa makamanda ni yale ambayo tumewafundisha vijana wetu tunaishi kama timu,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amesema sehemu ya mapato yatakayopatikana kutokana na shughuli za boti hilo itaenda kuchangia maduhuli ya serikali.
Hata hivyo ametoa rai kwa wadau wengine wanaohusika na masuala ya majini waendelee kutoa ushirikiano kwa kikosi cha 821 KJ Bulombora ili waweze kufikia malengo.
Kwa upande wake, Mkuu wa kikosi cha 821 KJ Bulombora Luteni Kanali Juma Hongo ameushukuru uongozi wa JKT kwa kulifanyia kazi wazo hilo.
"Tunawashukuru wadau wote waliohusika na kutupa ushauri kwani boti hii inamanufaa makubwa,"amesema Luteni Kanali Hongo.
"Katika matengenezo hayo kuna vitu vingi vimebadilishwa ikiwemo inji ya kisasa yenye uwezo mkubwa kwa gharama ndogo hata mabenchi yamekaa vizuri na majaketi yale ya kisasa yapo,"amesema.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akisalimiana mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa boti ya MV Bulombora iliyofanyiwa matengenezo makubwa na kikosi cha 821 KJ Bulombora hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza mara baada ya kuzindua boti ya MV Bulombora iliyofanyiwa matengenezo makubwa na kikosi cha 821 KJ Bulombora hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
Mkuu wa kikosi cha 821 KJ Bulombora Luteni Kanali Juma Hongo,akitoa taarifa kuhusu boti ya MV Bulombora iliyofanyiwa matengenezo makubwa na kikosi cha 821 KJ Bulombora hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa boti ya MV Bulombora iliyofanyiwa matengenezo makubwa na kikosi cha 821 KJ Bulombora hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiwa kwenye boti ya MV Bulombora mara baada ya kuizindua hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua boti ya MV Bulombora iliyofanyiwa matengenezo makubwa na kikosi cha 821 KJ Bulombora hafla iliyofanyika katika bandari ya Kigoma Mjini.
No comments:
Post a Comment