Faure Gnassingbé alikuwa rais baada ya kifo cha baba yake 2005 aliyeiongoza Togo kwa karibu miaka 40. |
Watu wa familia moja wamekuwa na historia ndefu kwa muda mrefu katika kuchagiza hali ya kisiasa ya mataifa mengi ulimwenguni.
Mfano, familia ya Bushes nchini Marekani hadi Kims huko Korea Kaskazini, Bhuttos nchini Pakistani hadi Trudeaus nchini Canada, majina fulani ya ukoo yamekuwa na nguvu na ushawishi wa kisiasa.
Nchini Togo, Afrika Magharibi, familia ya Gnassingbé imetawala kwa zaidi ya nusu karne, huku rais wa sasa, Faure Gnassingbé, yuko madarakani tangu 2005.
Akiendelea na mabadiliko ya katiba ambayo yanaweza kurefusha utawala wake, maswali yanaibuka kuhusu athari kwa demokrasia ya nchi hiyo.
Mabadiliko ya katiba ya 2002 yaliyoondoa ukomo wa mihula miwili ya urais yalisababisha maandamano makubwa Togo. |
Mwaka 1967, wakati rais wa sasa akiwa na umri wa miezi tisa tu, babake Gnassingbé Eyadéma alinyakua madaraka katika taifa hilo la Afrika Magharibi kupitia mapinduzi ya kijeshi.
Eyadéma alipofariki mwaka 2005, mwanawe Faure Gnassingbé akawa rais. Tangu wakati huo amekumbwa na maandamano makubwa, tishio la mapinduzi ya kijeshi na kupungua kwa umaarufu wa utawala wake.
Rais Gnassingbé anatazamiwa kusalia hadi 2031 baada ya Bunge la Kitaifa, linalotawaliwa na chama chake cha Union for the Republic (UNIR), kupitisha katiba mpya siku ya Ijumaa (19 Aprili) ambayo itabadilisha mfumo wa utawala wa nchi kwa rais na Wabunge.
"Kwa sasa hakuna mrithi wake anayeonekana. Rais haonekani kumpigia upatu mtu yoyote wa kumrithi kwa sasa," anasema msemaji wa Songhai Advisory, kampuni ya ushauri ya uwekezaji barani Afrika.
No comments:
Post a Comment