WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA TAALUMA YAO KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 1, 2024

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA TAALUMA YAO KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI


Na Okuly Julius Dodoma

Kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari ,waandishi wa habari wametakiwa kutumia taaluma yao kutoa elimu juu ya athari za uharibifu wa mazingira.

Rai hiyo imetolewa leo Mei 1,2024 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) , Kenneth Simbaya wakati akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutamatika kwa mbio maalum ikiwa ni sehemu ya shamrashamra kuelekea maadhimisho hayo.

Amesema maadhimisho ya mwaka huu yamekuja tofauti kwani inataka kuona mchango wa vyombo vya habari katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

"Tunalojukumu kubwa sana la kuhakikisha tunatunza Mazingira pale ambapo kuna uharibifu wa Mazingira madhara ni makubwa sana ukame,jangwa"

Na kuongeza kuwa "suala la Utunzaji wa Mazingira ni suala ambalo linapigiwa kelele na dunia nzima kwa hiyo sisi waandishi tukitumia kalamu zetu kupaza sauti tutakuwa tumetimiza wajibu wetu," ameeleza


Naye Afisa habari kutoka Umoja wa Mataifa Tanzania Nafisa Didi amesema kulingana na taarifa iliyotolewa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inaonesha Takwimu ndani ya miaka 15 zaidi ya waandishi 750 wanaofuatilia masuala ya mabadiliko ya tabianchi walipata madhara.

Amesema kuwa Umoja wa Mataifa huwa wanaongozwa na Shirika la Kimataifa la UNESCO katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani na Mpango kazi wao sasahivi katika mambo ambayo wanayafanyia kazi ni mabadiliko ya tabianchi.


"Kuna umuhimu wa kuzungumzia Kazi za utoaji wa taarifa zinazohusiana na mabadiliko ya tabianchi kwa sababu zinagusa waandishi wa habari hasa ambao wanafanya kazi eneo hilo na kuona ni namna gani tunaweza kuendelea kufanya kazi na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuweka Mazingira wezeshi ya kisera na kimipango"amesema

No comments:

Post a Comment