Na Saida Issa,Dodoma
SERIKALI imesema kuwa Kiwanda cha nyama cha Shinyanga ni miongoni mwa viwanda vitatu (3) vya nyama vilivyokuwa vinamilikiwa na Kampuni ya Tanganyika Packers Limited (TPL).
Kiwanda kilianza kujengwa 1975 na kilikamilika 1978 kwa asilimia 84% ila kiwanda hakijawahi kufanya kazi.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Alexnder Mnyeti alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Dkt.Christina Mnzava Je, Serikali ina mpango mkakati gani juu ya kiwanda cha nyama kilichopo Shinyanga ambacho hakifanyi kazi iliyokusudiwa.
"Mheshimiwa Spika, kiwanda cha nyama cha Shinyanga kilibinafsishwa kwa kampuni ya Triple S Beef Ltd, mwaka, 2007,
Hata hivyo, mwekezaji hakuweza kuendeleza kiwanda hicho kulingana na makubaliano ya mkataba wa ubinafsishaji jambo lililopelekea Serikali kuamua kukirejesha mwaka 2017 na kwa sasa kiwanda kipo chini ya usimamzi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina,"alisema.
Serikali inaendelea na juhudi za kutafuta mwekezaji mahiri mwenye nia thabiti ambaye atawekeza katika kiwanda hicho ili kiweze kufanya kazi iliyokusudiwa kwa maslahi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment