EVER AMWAGA WINO KUITUMIKIA AZAM. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 26, 2024

EVER AMWAGA WINO KUITUMIKIA AZAM.


Na Carlos Claudio.


Klabu ya Azam Fc imemtambulisha mchezaji Ever Meza kutoka klabu ya Leonnes ya nchini Colombia kuwa mchezaji mpya atakayewatumikia matajiri hao wenye maskani yao Chamazi.


Mchezaji huyo mwenye urefu wa 1.80m anacheza nafasi ya kiungo na ameonyesha uwezo mkubwa katika safu ya kiungo akitambulika kwa umahiri wake wa kupiga pasi na kusoma mchezo. 


Raia huyo wa Colombia ataanza kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu ujao kwa mkataba wa miaka minne utakaotamatika mwaka 2028.


Ever Meza amezaliwa Julai 21, 2000 na ameachana na klabu ya Alianza FC ya nchini Colombia aliyeitumikia kwa mkopo akitokea timu ya Leonnes kabla ya kuonyesha kiwango cha juu na kuvutia vilabu mbalimbali.


Azam FC imefanya uamuzi wa usajili huo muhimu kwa lengo la kuongeza nguvu katika kikosi chao na kuhakikisha wanapata mafanikio makubwa katika mashindano yote watakayoshiriki msimu ujao. 


Wanaamini kwamba Meza, kutokana na uzoefu wake wa kucheza katika ligi ya Colombia, ataleta ubunifu na ufanisi ambao utasaidia timu kufikia malengo watakayojiwekea.


Ujio wake katika miamba ya Chamazi unaleta matumaini makubwa kwa mashabiki na uongozi wa klabu ambao wanaamini kwamba Meza atachangia sana katika kampeni za timu za msimu ujao.




No comments:

Post a Comment