Ikiwa meneja wa Manchester United Erik ten Hag ataondoka, basi baada ya kipindi chake kizuri kwa muda wake akinoa timu hiyo, na Kombe la FA likinyanyuliwa mbele ya maelfu ya wachezaji wa kikosi cha ‘mashetani wekundu’ kwenye uwanja wa Wembley, ni njia nzuri ya kuondoka.
Ten Hag alitumia muda wa maandalizi ya shindano hili la mwisho dhidi ya mahasimu washindi wa mashindano yote Manchester City, akiwa amegubikwa na uvumi kwamba huu ungekuwa mchezo wake wa mwisho, meneja asiye na chake akitembea, na kusubiri tu mmiliki mwenza mpya wa United, Sir Jim Ratcliffe kumpa shinikizo la mwisho.
Manchester City walikuwa hapa kumletea fedheha ya mwisho kabla ya kuondoka, na kutoa kipigo cha mwisho na kushuhudia kocha huyu akishindwa.
Badala yake, katika mojawapo ya michezo ya kupendeza inayojitokeza mara nyingi, Ten Hag alionyesha ustadi wa kuifunga Manchester City 2-1, Mholanzi huyo aliinua miguu yake juu katika kusherehekea firimbi ya mwisho na mlinzi shujaa Lisandro Martinez kabla ya kwenda kushirikishana naye tukio la kipekee, kumpa mkono wa faraja Pep Guardiola aliyechabangwa.
Kiwango cha mafanikio ya United wakati presha ilipokuwa juu zaidi kwa meneja na wachezaji ni kwamba hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa City kupoteza, mbali na mikwaju ya penalti dhidi ya Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, tangu waliposhindwa na Aston Villa mnamo Disemba 6.
Iwapo hii inaleta tofauti yoyote kwa watoa maamuzi wa Old Trafford, wakiongozwa na Ratcliffe, bado ni jambo linalosubiriwa lakini kwa mateso yake yote na ukosoaji ambao amekumbana nao - mengi ya hayo yalihalalishwa baada ya msimu mbaya kama huo - Ten Hag alifurahia kipindi hiki akiwa Wembley.
Mmiliki mwenza wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe akisalimiana na meneja Erik ten Hag baada ya ushindi wa fainali ya Kombe la FA. |
Ratcliffe na muundo wake mpya wa kandanda hauwezekani kuunda mustakabali wa baadaye kwa kuzingatia mchezo mmoja, haijalishi ni wa sifa kiasi gani, na swali la msingi linaweza kuulizwa ni, imekuwa wapi United ambayo iliicharaza City, haswa mchezo wa kipindi cha kwanza kilichosisimua, kwa msimu wote huu?
Taarifa ya baada ya mechi iliyotolewa na Ratcliffe haikuwa vidokezo vyovyote kuhusu mustakabali wa Ten Hag lakini pia, haikutoa chochote cha msingi kwa umma, ambacho kilionekana muhimu.
Jibu la meneja huyo, kama ilivyokuwa siku zote, ni kusema kwa usahihi kwamba alirithi klabu na timu ambayo mtangulizi wake Ralf Rangnick alidai ilihitaji "upasuaji wa moyo".
Pia alitaja orodha ndefu ya majeruhi, akisema baada ya ushindi wa United: “Nawaambia hivi mwaka mzima. Wachezaji wanapokuwa sawa tunaweza kucheza soka nzuri sana. Huu ulikuwa mchezo mzuri sana dhidi ya timu bora zaidi duniani.
"Nadhani ukosoaji haukuwa wa haki, kwa timu na mimi pia. Haikuwa sawa. Hatukuwa na wachezaji.
Tumeona mambo yale yale, ukosefu wa soka nzuri kila wakati – hapana, sio hivyo - lakini tulilazimika kujifinya kila wakati na matokeo yake, huwezi kucheza mpira unaotaka.
"Nilikuwa na kikosi kamili labda mara tatu au nne katika miaka miwili. Hata hapa tulikosa wachezaji wakubwa kama Harry Maguire, Luke Shaw na Casemiro.”
Mchezaji bora wa mechi Kobbie Mainoo akishangilia na Kombe la FA baada ya Manchester United kushinda Wembley. |
Hoja zote ni sawa lakini zikidhoofishwa na ukosefu wa mkakati na udhibiti mara nyingi sana, na kampeni ya Ligi ya Mabingwa ambayo haikuwa na hadhi na sifa zake, United hata haikutoka katika hatua ya makundi.
Na hakika, United hawakutumia uzoefu na ustadi wao hadi kushinda Kombe la FA kwa mara ya 13.
Walipoteza uongozi wa mabao mawili kwa moja kabla ya kulaza Newport County katika raundi ya nne na kupata ushindi mkubwa wa 4-3 dhidi ya Liverpool katika robo fainali kwa bao la Amad Diallo katika sekunde za mwisho za muda wa nyongeza, kabla ya kuepuka aibu kubwa kwenye nusu fainali, ikiitoa kwa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Championship Coventry City.
Ushindi huu wa kipekee dhidi ya mabingwa hao mara nne wa Ligi ya Primia ulikuwa wa kawaida lakini hakuna kilichobadilika katika mpangilio wa Ten Hag ambao uliwaletea mabao mawili muhimu kipindi cha kwanza.
Na ukweli kwamba walifungwa na vijana Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo utaleta furaha zaidi, kwa United, klabu ambayo daima imekuwa ikithamini vipaji vya vijana.
Bao la Mainoo lilikuwa la kipekee, krosi nzuri kabisa ya Marcus Rashford ikimpata Garnacho, ambaye krosi yake ilifikiwa na mguso mwembamba na kuona vizuri kwa Bruno Fernandes.
Mainoo, akiwa na umri wa miaka 19 pekee, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kuonyesha ukomavu na udhibiti wa hali ya juu, na hivyo kudhihirisha kuwa ana tabia ya kucheza mechi kubwa dhidi ya wapinzani bora - ambayo itatiliwa maanani na meneja wa Uingereza Gareth Southgate kabla ya Euro 2024.
Pia unaweza kuona ilimaanisha nini kwa Rashford baada ya wiki mbaya ambapo kudorora kwake msimu huu kulitokana na uamuzi wa Southgate wa kumtoa fowadi huyo kutoka kwa kikosi cha muda cha wachezaji 33 cha England kwa ajili ya dimba la Ujerumani.
Rashford alitokwa na machozi wakati wa sherehe za United na mashabiki wao baada ya kukabidhiwa Kombe la FA.
No comments:
Post a Comment