HISIA KALI YENYE FURAHA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 10, 2024

HISIA KALI YENYE FURAHA.

 


Mchezaji na beki wa kulia wa Simba SC David Kameta "Duchu" akiwa na furaha iliyopitiliza baada Ya kuipatia timu yake goli la tatu kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC.


Kijana huyo aliingia kutoa benchi kuchukua nafasi Ya Edwin Balua na alifanikiwa kufunga goli la 3 na kushangilia kwa hisia kali sana na kudondosha chozi baada Ya kufunga.



Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Kameta bada Ya kufunga goli ilo akiwa amelala chini.



Katika mchezo huo mkubwa ambao umeonyesha maana halisi ya Derby ya Mizima uhasama wa timu mbili ambazo zinamilikiwa na matajiri wawili wakubwa nchini, mmoja akiwa mmiliki na mwingine akiwa Mwekezaji wa timu hiyo.

Kipindi cha kwanza kilionyesha uhalisia na ubora wa Azam FC kwa msimu huu kivipi, kwa Simba SC kukubali kuwa timu ya pili kiwanjani kwa kuingia huku wakiwaheshimu Azam Fc kuwa wao ni bora zaidi yao na ndiyo maana wachezaji wa Simba SC muda mwingi walikuwa chini wakiwazuia Azam FC.

Azam FC walikuwa bora sana kuanzia kuzuia mashambulizi pamoja na kutengeneza mashambulizi kuanzia nyuma, uwezo wa wachezaji wengi wa Azam Fc kwenye kumiliki mpira Iddy Nado, Kipre Junior na Gibril Sillah jambo ambalo liliwapa nafasi zaidi ya kukabia juu ili kuweza kupunguza hatari kwenye lango lao.


Simba SC walilitambua na kuamua kukabia katikati zaidi licha ya Azam FC wakifika katikati ya uwanja na wachezaji wa Simba SC walikuwa haraka zaidi kuwazuia Azam FC.





No comments:

Post a Comment