JESHI LA POLISI LIBADILIKE, LIENDANE NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA- DKT. MPANGO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 11, 2024

JESHI LA POLISI LIBADILIKE, LIENDANE NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA- DKT. MPANGO.


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesisitiza jeshi la polisi kubadilika katika mbinu na ubunifu wa matumizi ya TEHAMA ili kukabiliana na mbinu mpya za kiuhalifu kupitia mafunzo ya intelejensia, usalama na uhalifu wa kimtandao.

 

Hayo yamesemwa leo Mei 11,2024 jijini Dodoma katika ufunguzi wa kituo cha polisi daraja A” wilaya ya Kipolisi Mtumba na kukabidhi magari 21 kwa jeshi la polisi.

 

Amesema ukuaji kwa maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi umechangia shuguli nyingi mtandaoni na hali hiyo imewafanya wahalifu pia kutafuta mbinu za kufanya uhalifu kupitia mitandao hivyo jeshi la polisi linatakiwa kubadilika kwa haraka zaidi ili kuweza kukabiliana na hizo mbinu mpya za uhalifu.

 

Ajali za barabarani ambazo zinaweza kuepukika bado zinaangamiza watanzania na sehemu kubwa ya ajari hizi ni zile ambazo zinasababishwa na ubovu wa magari, kutozingatia sheria za usalama barabarani na madereva kukosa weledi.

 

Dkt. Mpango amesema, Maadili mema na nidhamu kazini pamoja na uwajibikaji ni nguzo muhimu kwa jeshi la polisi katika kusimamia sheria, ninatambua vizuri maboresho yanayoendelea katika jeshi la polisi na juhudi mbalimbali za wizara za jeshi lenyewe kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake.

 

Aidha amelieleza jeshi la polisi lielekeze zaidi katika kubuni na kutumia mifumo ya TEHAMA kuhakikisha askari na makamanda wanapata mafunzo ya mara kwa mara kwenye maeneo ya Intelijensia,  usalama na uhalifu wa kimtandao pamoja na matumizi ya akili mnemba na roboti.

 

Hata hivyo amebainisha kuwa jeshi la polisi kuangalia upya mfumo mzima wa utoaji leseni za kuendesha vyombo vya moto, ukaguzi wa magari, matumizi ya teknolojia ikiwemo camera za barabarani ili kudhibiti rushwa barabarani na kuimarisha weledi na udhibiti wa vyombo vya moto.

 

Dkt. Mpango ameongeza kuwa jeshi la polisi linapaswa kujenga uhusiano mzuri kati yake na wananchi kwani uhusiano huo utawezesha wananchi kuendelea kushiriki katika kufichua na kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kuwa wahalifu ni sehemu ya jamii.

 

Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi IGP Camillius Wambura amesema kituo hiko kitahudumia jumla ya kata 8 zilizomo ndani ya wilaya ya Dodoma mjini ambazo ni wilaya ya Homboro Bwawani, Homboro Makuru, Kikombo, Ihumwa, Chawa, Ipala, Mtumba na Chihanga ambazo kata hizo zimejumuhishwa na kupewa hadhi ya wilaya ya Kipolisi Mtumba zenye wakazi wapatao 108,377.

 

Serikali kuendelea kutujengea vituo hivi vya daraja A” na madaraja mengine ikiwemo kutupatia vitendea kazi kama haya magari, imetuwezesha jeshi la polisi kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi zaidi na kupunguza uhalifu na kuwapa fursa wananchi kushiriki katika shuguli za maendeleo bila hofu ya uhalifu mkubwa,” amesema IGP Wambura.

 

Amesema ujenzi wa kituo cha polisi Mtumba ulianza  tarehe 7 Julai, 2021 na uwekaji wa jiwe la msingi ulifanywa tarehe 2 Disemba, 2021 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

 

Nae Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ulinzi na mambo ya nje Mhe. Victor Kawawa amesema serikali imejenga vituo vya polisi hivyo vinatakiwa vitunzwe ili viendelee kutimiza malengo yake ya kujengwa ni lazima vifanye kazi kikamilifu, pia ameshauri mfumo wa kufungua kesi mtandaoni ufunguliwe katika vituo vingi zaidi kwani mpaka sasahivi ni vituo 26 vinavyotoa huduma hiyo ikiwemo kituo kipya cha wilaya ya Kipolisi Mtumba.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde amesema kumekuwa na ushirikiano mkubwa wa jeshi la polisi pamoja na wananchi wa jimbo la Dodoma mjini na wanaunga mkono jitihada kubwa za jeshi la ulinzi na usalama wa raia na mali zake kwani wananchi wa Dodoma mjini wamejitokeza sana katika ujenzi wa vituo vya polisi vinavyojengwa katika kata ya Ihumwa, Mpunguzi na Changombe, lakini kupitia uzinduzi wa kituo hiko cha wilaya ya Kipolisi cha Mtumba kitatatua huduma kwa wananchi zaidi ya laki 1 wa kata 8 ambao hapo awali walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma.









No comments:

Post a Comment