Ripoti ya hivi karibuni, inaeleza kuwa mauzo ya bidhaa za Apple yamepungua kote ulimwenguni, mauzo hayo yamepungua katika nchi zote isipokuwa Ulaya.
Kampuni hiyo ilisema mahitaji ya simu zake za kisasa yamepungua kwa asilimia 10 katika miezi mitatu iliyopita ya mwaka huu.
Apple imeripoti mapato jumla ya kampuni hiyo yamepungua kwa asilimia nne hadi dola bilioni 90.8. Huu ni upungufu mkubwa katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.
Lakini matokeo hayakuwa mabaya kama ilivyotabiriwa. Kwa upande mwingine, hisa za Apple ziliongezeka katika soko huko New York.
Kampuni hiyo inasema kushuka huko kulitokana na changamoto katika usambazaji kutokana na janga la Covid 19.
Inatarajia mauzo kuongezeka tena, ikiamini yataboreka katika siku za usoni kufuatia uzinduzi wa bidhaa mpya na uwekezaji katika akili bandia.
Mauzo jumla katika soko kuu la China yalishuka kwa asilimia 8.
Mkurugenzi Mtendaji wa Apple Tim Cook, aliwahakikishia wawekezaji kuwa mauzo ya iPhone yameanza kuongezeka China bara. Alisema ana matarajio makubwa na China.
“Kwa kweli, Apple inapata ushindani kutoka makampuni ya ndani kama Huawei,” anasema mchambuzi wa teknolojia kutoka kampuni ya DA Davidson, Gil Luria, “kampuni kama Huawei zinafanya vizuri nchini China kwa sababu ni chapa yao ya nyumbani."
Alisema katika kipindi cha BBC kuwa iPhone ni bora kuliko simu zingine za kisasa katika suala la sifa zake, utendaji na heshima.
"Kwa hivyo wakati wowote wateja wana chaguo na wakiwa na rasilimali za kifedha watanunua iPhone," anaelezea.
Apple inapata ushindani kutoka makampuni ya ndani kama Huawei. |
Mauzo ya simu janja duniani yalipanda kwa asilimia 10 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka. Kulingana na kampuni ya utafiti ya Canalys, ongezeko hili lilikuja baada ya muda mrefu kupita.
Luriat anasema tangu iPhone 12 iliyotoka takriban miaka minne iliyopita, hakujakuwa na uboreshaji mkubwa katika simu za Apple. Lakini baada ya Apple kuzindua 5G iliwavutia wateja.
"Wanatumai wanaweza kuleta vipengele vipya vya akili banda kwenye iPhone 16, ambayo vinaweza kuwepo mwishoni mwa mwaka huu, na baada ya hapo awamu kubwa ya uboreshaji wa iPhone inaweza kuanza," alisema.
Apple pia inakabiliwa na vita vya kisheria na wadhibiti nchini Marekani na Ulaya kuhusu ada zake za App Store. |
Kuna kesi nchini Marekani ambapo Google inahoji malipo makubwa ambayo Apple inapokea kutoka kwa kampuni kubwa.
Malipo hayo yalikuwa na thamani ya takriban dola bilioni 20 mnamo 2022, kulingana na faili za korti, malipo yaliyosaidia kuongeza faida kwa Apple.
Faida ya kabla ya kodi kwa miezi mitatu ilikuwa dola bilioni 28 na kampuni hiyo ilitangaza kuwa ilikuwa ikitenga dola 110 bilioni kununua hisa.
Mkuu wa fedha Luca Maestri alisema mauzo ya Apple yanatarajiwa kukua katika kipindi cha miezi mitatu kufikia Juni.
Aliongeza kampuni hiyo inatarajia ukuaji wa tarakimu mbili katika biashara yake.
"China inafanya vizuri zaidi kuliko ilivyotarajiwa na kuna fursa nyingi mbeleni ambazo zinaweza kuboresha hisia za wawekezaji," alisema Angelo Zino, mtafiti wa kampuni ya utafiti ya CFRA.
No comments:
Post a Comment