Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Mhe. David Mathayo ameuliza swali la nyongeza kwa waziri wa aridhi Mhe. Jerry Slaa kuwa lini atakwenda kutatua kero na migogoro ya aridhi inayoendelea katika kijiji cha Bangalala tarafa ya Mwembe- Mbango kata ya Makaya na Ruvu katika wilaya ya Same ambayo inapelekea kukwamisha maendeleo ya wananchi hasa katika kipindi hichi cha kilimo na ufugaji.
"Nikuombe Mhe waziri naomba tuongozane pamoja baada ya vikao vya bunge kumalizika kwenda kutatua migogoro hiyo ambayo imedumu zaidi ya miaka 19 bila ya ufumbuzi wowote na kupelekea wananchi kutoelewana na kusimamisha shughuli za maendeleo katika maeneo hayo lengo wananchi hao waweze kuishi kwa amani na upendo kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi,”amesema Mathayo.
Waziri mwenye dhamana ya aridhi Mhe. Jerry Slaa amekiri kuambatana na mbuge wa jimbo la Same Magharib Mhe. David Mathayo mara baada ya kumaliza kuwasilisha bajeti yake ya wizara ya Aridhi ifikapo mwezi June,2024 kwenda kutatua migogoro hiyo ambayo inaendelea katika kipindi hiki.
"Mhe Naibu Spika niombe radhi kwa wananchi wa Same hasa wa jimbo la Same Magharibi ambapo nilifanya ziara January 26 na kutembelea sehemu ya migogoro hiyo kata ya Bangalala Makanya na Ruvu na pia nikatuma wataalam kuja kupima maeneo na mipaka, nimeshawasilishiwa ofisini hivyo baada ya kumalizika Kwa vikao vya bunge ntaongozana na Mhe David Mathayo kwenda kutatua migogoro hiyo,” amesema Mhe Jerry Slaa.
No comments:
Post a Comment