Baadhi ya Nyumba zilizozingirwa na Maji katika eneo la Mtaa wa Maweni Bondeni kata ya Mji Mwema Wilaya ya Kigambini mkoa wa Dar es Salaam. |
Baadhi ya Nyumba zilizozingirwa na Maji katika eneo la Mtaa wa Maweni Bondeni kata ya Mji Mwema Wilaya ya Kigambini mkoa wa Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU) |
Na Mwandishi wetu.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala tarehe 9 Mei, 2024 amefanya ziara ya kutembelea Wilaya ya Kigamboni kata ya Mjimwema Mtaa wa Maweni kwa lengo la kuangalia madhara yaliyotokea kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.
Awali akiwa katika kikao cha pamoja na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Ndg. Chillah Moses katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya madhara ya mvua hizo kwa Wilaya ya Kigamboni alielezwa kuwa maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Mtaa wa Maweni eneo la Bondeni kata ya Mji Mwema pamoja na Maweni eneo la Biasi ambayo yamezingirwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo.
Aidha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu itaendelea kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na stahimilivu dhidi ya maafa.
No comments:
Post a Comment