MAAFISA USHIRIKA SIKONGE WASHTAKIWA KWA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 25, 2024

MAAFISA USHIRIKA SIKONGE WASHTAKIWA KWA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA.



KUTOKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI TABORA.


Mei 24, 2024 Ofisi ya TAKUKURU (W) Sikonge mkoani Tabora kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (M) Tabora, imewafikisha mahakamani washtakiwa wawili EMMANUEL ADO HYERA na MICHAEL EMMANUEL NGUSA. 


Washtakiwa hawa ambao ni Maafisa Ushirika wa Wilaya ya Sikonge wamefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi Na. (ECO:13092/2024).


Kesi imesomwa mbele ya Mh. NGAEJE (SRM) ambapo washtakiwa wote wawili wanashtakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na kifungu cha 31 cha PCCA [sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022]. Kwamba, maafisa hao walitumia mamlaka yao kufanya biashara haramu ya kulangua tumbaku bila kuwa na leseni kinyume na kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Tobacco Industry Act ya  Mwaka 2001 na kujipatia faida. 


Aidha Jamhuri imewasilisha maombi ya kuzuia mali za washtakiwa kwakua zinahusiana moja kwa moja na makosa yao. 


Washtakiwa wote wamekana mashtaka yao na wameachiwa kwa dhamana. Kesi itakuja tena Mei 28, 2024 kwa kutaja hoja za awali na Mei 27, 2024 kwa ajili ya kupata uamuzi mdogo wa maombi ya zuio.

No comments:

Post a Comment