MICHEZO IPEWE KIPAUMBELE KWA WATUMISHI WA WIZARA NA TAASISI: BASHUNGWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 1, 2024

MICHEZO IPEWE KIPAUMBELE KWA WATUMISHI WA WIZARA NA TAASISI: BASHUNGWA


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, kuhakikisha anawezesha Watumishi wa Wizara na Taasisi zake kushiriki kikamilifu katika michezo na mashindano ya kimichezo yanayoandaliwa kwa ajili yao.

Bashungwa ametoa agizo hilo leo, Mei 1, 2024, Mkoani Arusha, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi mara baada ya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi. Amesisitiza Watumishi wa Wizara na Taasisi zake kushiriki katika michezo na mashindano ya Mei Mosi na matukio mengineyo.


“Mimi ni mpenzi wa michezo na mwanamichezo pia. Nimuelekeze Katibu Mkuu wa Ujenzi kuwawezesha Watumishi wa Wizara na Taasisi zake kushiriki mashindano haya kila mwaka na kufanya michezo iwe kipaumbele kama majukumu mengine yetu,” amesisitiza Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu pamoja na Wakuu wa Taasisi kutenga bajeti kwa ajili ya Watumishi wenye vipawa vya michezo mbalimbali, pale inapobidi kwa michezo inayoratibiwa na Serikali, na kuwapatia vibali ili waweze kushiriki.

Bashungwa ameeleza kuwa ushiriki wa michezo ya Mei Mosi ni moja ya wajibu wa Serikali, hivyo hakuna budi kwa Mtumishi yeyote wa Serikali kunyimwa nafasi hiyo.

Pia, Bashungwa ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa Wizara na Taasisi zake kuanza kujipanga na kujiandaa vizuri kwa ajili ya kushiriki michezo ya Mei Mosi mwaka ujao.

Halikadhalika, Bashungwa ameendelea kuwasisitiza Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake kutanguliza Uzalendo na maslahi ya Taifa mbele wakati wa kutekeleza majukumu yao.

No comments:

Post a Comment