SERIKALI imesema imeongeza udahili katika vyuo vya elimu ya ufundi kutoka wanafunzi 171,581 mwaka 2022/23 hadi wanafunzi 235,804 mwaka 2023/24.
Hayo yamebainishwa leo Mei 7, 2024 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2024/2025
"Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa idadi ya vyuo vya elimu ya ufundi kutoka vyuo 465 (visivyo vya serikali 285) mwaka 2022/23 hadi vyuo 474 (visivyo vya serikali 294) mwaka 2023/24," -Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
##OKULYBLOGUPDATES##
No comments:
Post a Comment