VIPAUMBELE VITANO SEKTA YA ELIMU VYATAJWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 7, 2024

VIPAUMBELE VITANO SEKTA YA ELIMU VYATAJWA


SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanikiwa kutekeleza vipaumbele vitano katika mwaka wa fedha 2023/24 ambavyo ni pamoja na kukamilisha Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na Mitaala ya Elimu na kuanza utekelezaji wake kwa lengo la kuimarisha ujuzi kwa wahitimu.

Hayo yamesemwa leo Mei 7, 2024 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2024/2025.

Prof Mkenda amesema wamefanikiwa kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa mafunzo ya amali kwa sekondari na vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, kuwezesha Ongezeko la fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.

Amesema vipaumbele vingine ni kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuimarisha uwezo wa nchi katika tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.

#okulyblogupdates

No comments:

Post a Comment