SERIKALI KUENDELEA KUKUZA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, May 7, 2024

SERIKALI KUENDELEA KUKUZA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA


SERIKALI imesema imeendelea kuimarisha udhibiti na kukuza matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa kutekeleza mambo kadhaa ikiwemo usajili wa vituo vipya 43 vya Mionzi ayonishi na kufikisha jumla ya vituo vya mionzi 1,386 vilivyosajiliwa na vituo vipya 42 vya mionzi isiyoayonishi na kufikisha jumla ya vituo vya mionzi isiyoayonishi 409 vilivyosajiliwa.

Hayo yamebainishwa leo Mei 7, 2024 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara hiyo.


Amesema Serikali imesajili vyanzo vipya 36 vya mionzi na kufikia jumla ya vyanzo vya mionzi 1,647 vilivyosajiliwa

"Serikali imetoa leseni 633 za kumiliki na kutumia vyanzo vya mionzi, uingizaji nchini wa vyanzo vya mionzi 95, utoaji nje ya nchi wa vyanzo vya mionzi 13 na safirishaji wa vyanzo vya mionzi ndani ya nchi 47; imepima viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 1,980 wanaofanya kazi katika vyanzo vya mionzi katika vituo 429 


"Aidha, viwango vya mfiduo vilivyopokelewa katika miezi mitatu mfululizo vilianzia 0.1 hadi 3.2 millisievert (mSv), ambavyo viko ndani ya ukomo unaokubalika wa udhibiti", amesema Prof Mkenda.

#okulyblogupdates 

No comments:

Post a Comment