Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma siku ya Alhamisi aliikosoa mahakama ya juu ya nchi hiyo na washirika wake wa zamani katika chama tawala cha African National Congress.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma siku ya Alhamisi aliikosoa mahakama ya juu ya nchi hiyo na washirika wake wa zamani katika chama tawala cha African National Congress kwa kunyimwa haki yake ya kushiriki uchaguzi wa wiki ijayo na kusema kuwa atapigania haki zake "kwa njia yenye nidhamu."
Maoni ya Zuma yalitolewa katika ujumbe wa video ambao alisema ulilenga watu wa Afrika Kusini na kutolewa kwenye mitandao ya kijamii siku sita kabla ya kura hiyo ya kitaifa.
Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 82 aliweka wazi kuwa bado atafanya kampeni dhidi ya ANC aliyokuwa akiiongoza wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa Jumatano na chama chake kipya cha siasa, ingawa amezuiwa kugombea nafasi ya kurejea bungeni miaka sita baada ya kujiuzulu urais chini ya wingu la tuhuma za ufisadi.
No comments:
Post a Comment