Na Okuly Julius,Dodoma
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wanawake waliohitimu mafunzo ya udereva kuchangamkia fursa za ajira serikalini kwani muitikio wa wanawake katika nafasi hiyo ni mdogo.
Senyamule ameyasema hayo Mei 11, 2024 jijini Dodoma, wakati akifunga mafunzo na kutunuku vyeti vya udereva kwa wanawake zaidi ya 180 yaliyoandaliwa na chuo cha udereva cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING.
"Niwaambie tu serikali ina Sera yake ya ajira ambayo katika kile ajira inataka asilimia 30 wawe ni wanawake ila huku kwenye udereva hata asilimia 10 bado haijatumika hivyo kwa kuhitimu kwenu mafunzo hayo ni vyema mkawa na uthubutu muombe nafasi za udereva serikalini pindi zinavyotangazwa," ameeleza Senyamule
Pia Senyamule ametoa wito kwa wanawake hao kuanzisha umoja wa madereva wanawake ili kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali kupitia halmashauri
Amesema Umoja huo utawawezesha kupata mikopo hiyo ya asilimia 10 na ikiwezekana wanunue mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi kwani mbali na mwanamke kuwa dereva ataendelea kusimama kama mlezi hivyo wazazi wengi na shule nyingi zitatamani kukodisha mabasi yao kwa ajili ya kupeleka wanafunzi shule na kurudisha nyumbani kwa wanawake wanaaminika katika jamii.
Pia Senyamule amikipongeza Chuo cha WIDE kwa kuendesha mafunzo hayo na kutoa vyeti kwa wanawake hao bila malipo jambo ambalo hakuna mwekezaji yeyote aliyeweza zaidi ya chuo hicho.
"Hakuna mwekezaji yupo tayari kupoteza zaidi ya milioni 37 kuwasaidia watu tena kupata mafunzo ila nyinyi WIDE mmeonesha mfano mzuri na wakuigwa na wawekezaji wengine kurudisha kidogo kwa jamii,"amesema Senyamula
Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo cha udereva cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING Faustine Matina ameelezea sababu za chuo hicho kutoa mafunzo hayo kwa wanawake kuwa wametaka kuionesha jamii nguvu aliyonayo mwanamke na kuondoa ile dhani kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu huku akibainisha kuwa wanawake hao wamepata ujuzi wa kutosha kuendesha hata mabasi l.
"Jamii zetu bado zinawadharau wanawake na kuwaona kama hawawezi ila sisi kama WIDE tumeamua kumshika mkono mwanamke kuidhihirishia jamii kuwa hakuna kazi inayomshinda mwanamke kikubwa ni aungwe mkono,
Na kuongeza kuwa "niwaombe wahitimu wote mtusaidie kuwa mabalozi wema huko katika jamii zenu ili wengine nao wapate fursa ya kuja kusoma kwani elimu ya udereva ni elimu muhimu sana kwa kila mmoja," ameeleza Matina
Nao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameeleza changamoto zinazopelekea wanawake wengi kutochangamkia fursa huku wakisema wanaume wengi hawapendi kuona wake zao wakisomea tasnia hiyo ya udereva.
No comments:
Post a Comment