Na Okuly Julius , Morogoro
Hayo yameelezwa leo Mei 13,2024 Mkoani Morogoro na Mhasibu Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha CPA Jenipha Ntangeki wakiti akitoa wasilisho kuhusu masuala ya PENSHENI na Mirathi kwenye semina na waandishi wa habari wa mitandaoni na kuongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kila mstaafu anahudumiwa alipo bila usumbufu wowote.
“Katika kutatua changamoto hii Serikali imeendelea kutoa elimu kwa Umma kupitia vyombo mbali mbali vya habari kama tunavyofanya hapa leo, na hii ni kwa kutambua umuhimu wenu wana habari kwa jamii kwa ujumla ,nyumba za ibada, Kupitia Wahariri, maonesho ya Sabasaba, Nanenane na wiki ya Watumishi wa Umma na wiki ya huduma za kifedha,”amesema.
Amesema elimu ni vyema kuendelea kutolewa kwa Wastaafu na Wastaafu watarajiwa kwani kustaafu kunakuja ghafla hivyo ni vyema kila mmoja kujiandaa.
“Kwa nini tunasema kustasfu ni ghafla, kustaafu maana yake ni kushindwa kupata kile kipato ambacho umekuwa ukikipata siku zote na kuna sababu nyingi tu za kumfanya mtu astaaafu au astaafishwe ukiachilia mbali wale wanaostaafu kwa hiari wakiwa na miaka 55 na wale wanaostaafu kwa lazimi wakifikisha miaka 60 ila kuna wale wanaositishiwa mikataba kutokana na kukiuka taratibu au utovu wa nidhamu ikiwemo pia maradhi hayo yote yanaweza kusababisha mtu astaafu ghafla,” ameeleza CPA Jenipha.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini wizara ya fedha Benny Mwaipaja amesema kuwa Wizara ya Fedha inaendelea kuwakumbusha wastaafu kutojihusisha na utoaji wa fedha zozote kwa mtu au watu kwa kigezo cha kusaidiwa kupata PENSHENI,kwani wizara hiyo haiombi fedha ili kuwasaidia wastaafu.
"Lengo la kufanya haya ni kutaka kuwasaidia wastaafu hawa na familia zao wasiendelee kutapeliwa kwani kwasasa haya matukio yamekuwa yakiongezeka unakuta mtu kakaa zake mezani anapiga simu kuomba fedha kwa mstaafu ili amtumie help amsaidie kwahiyo naamini kupitia kwenu hawa watu tutaweza kuwasaidia,"amesema.
Aidha amesema kuwa wanahabari ni muhimu sana kuwashirikisha katika suala hilo kutokana na namna ambavyo teknolojia inazidi kukuwa zaidi na wahalifu wanabuni njia za kutaka kuwatapeli wastaafu.
Kwa upande wake Mwenyejiti wa mafunzo hayo Mathias Canal ameipongeza Wizara ya fedha kwa kuandaa mafunzo hayo yenye lengo la kuwaongezea uzoefu wanahabari haonl pamoja na kuwasaidia wastaafu kuepukana na changamoto wanazozipitia kipindi cha kudai pensheni zao.
No comments:
Post a Comment