WIZARA YA FEDHA YAWATAKA WASTAAFU KUWAPUUZA MATAPELI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 13, 2024

WIZARA YA FEDHA YAWATAKA WASTAAFU KUWAPUUZA MATAPELI

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini , Wizara ya Fedha Benny Mwaipaja , akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari za mitandaoni leo Mei 13,2024 Mkoani Morogoro.

Na Okuly Julius , Morogoro

Wizara ya Fedha imeendelea kuwakumbusha wastaafu kutojihusisha na utoaji wa fedha zozote kwa mtu au watu kwa kigezo cha kusaidiwa kupata PENSHENI,kwani wizara hiyo haiombi fedha ili kuwasaidia wastaafu.

Hayo yameelezwa leo Mei 13,2024 Mkoani Morogoro na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini , wizara ya fedha Benny Mwaipaja wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari za mitandaoni huku akiwaomba pia kuwa mstari wa mbele katika kukumbushia suala hilo.

"Lengo la kufanya haya ni kutaka kuwasaidia wastaafu hawa na familia zao wasiendelee kutapeliwa kwani kwasasa haya matukio yamekuwa yakiongezeka unakuta mtu kakaa zake mezani anapiga simu kuomba fedha kwa mstaafu ili amtumie help amsaidie kwahiyo naamini kupitia kwenu hawa watu tutaweza kuwasaidia,"amesema.

Aidha amesema kuwa wanahabari ni muhimu sana kuwashirikisha katika suala hilo kutokana na namna ambavyo teknolojia inazidi kukuwa zaidi na wahalifu wanabuni njia za kutaka kuwatapeli wastaafu.

Kwa upande wake Mwenyejiti wa mafunzo hayo Mathias Canal ameipongeza Wizara ya fedha kwa kuandaa mafunzo hayo yenye lengo la kuwaongezea uzoefu wanahabari hao pamoja na kuwasaidia wastaafu kuepukana na changamoto wanazozipitia kipindi cha kudai PENSHENI zao.

No comments:

Post a Comment