SERIKALI KUENDELEA KUOBESHA MIUNDOMBINU YA AFYA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 24, 2024

SERIKALI KUENDELEA KUOBESHA MIUNDOMBINU YA AFYA.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange (Mb) amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Afya nchini Kote ili kuendelea kuwasaidia na kuwahudumia Wananchi katika maeno mbali mbali

Mhe. Dkt.Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Jackson Gidion Kiswaga Mbunge wa Jimbo la Kalenga aliyeuliza Je Serikali haioni haja kuunga mkono jitihada za Wananchi wa Kalenga katika ujenzi wa kituo cha Afya cha Kibena.

“kupitia mradi wa usafi wa mazingira serikali ilitoa mil. 74.9 kwaajili ya uboreshaji wa vyoo, mifumo ya maji safi na maji taka Pamoja na ujenzi wa kichomea taka, ambapo maboresho ya miundombinu hiyo imekamilika na inatumika” Dkt. Dugange.

No comments:

Post a Comment