SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 16, 2024

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali kuhusu matumizi ya mashine za kutolea risiti kwa njia ya kielektroniki (EFD), bungeni jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)

Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.

Serikali imesema kuwa taratibu za kikodi zimebainisha kwamba, mfanyabiashara yeyote mwenye mauzo ghafi yenye kiasi cha shilingi milioni kumi na moja (TZS 11,000,000) na kuendelea kwa mwaka, anapaswa kutumia mashine za kutoa risiti za kielekroniki (EFD) kwa walipakodi wote wanaofanya biashara mara nyingi au mara moja kwa mwaka.


Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi Mhe. George Mwenisongole, aliyetaka kujua ni kwa nini TRA inalazimisha Vyama vya Msingi vya Ushirika kutumia EFD mashine wakati hawafanyi biashara na mauzo yao ni mara moja kwa mwaka.

 

Mhe. Dkt. Nchemba alisema lengo kubwa la Serikali la kuanzisha matumizi ya mashine ya EFD ni kuhamasisha na kujenga utamaduni wa kutunza kumbukumbu za biashara na kwamba EFD, inahakikisha dhana ya uwazi inasimamiwa kikamilifu.

‘‘Kifungu namba 36 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Act) ya mwaka 2015 kinaelekeza kwamba, “mtu yoyote anayesambaza bidhaa, kutoa huduma au kupokea malipo kuhusu bidhaa au huduma anazosambaza anatakiwa kwa mujibu wa sheria kutoa risiti za mashine za kieletroniki kulingana na kiasi cha fedha alichopokea kutokana na bidhaa au huduma aliyotoa’’, alifafanua Mhe. Dkt. Nchemba.

Aliongeza kuwa Mashine ya EFD ni kati ya vifaa ambavyo humsaidia mfanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara kwa muda mrefu, na kwa upande mwingine huisaidia Serikali kutambua mauzo na kutoza kodi stahiki pale inapopaswa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment