TANROADS KAZINI KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA DAR - LINDI - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Sunday, May 5, 2024

TANROADS KAZINI KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA DAR - LINDI


Timu ya Watalaamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakandarasi wanaendelea na kazi ya kurejesha miundombinu ya Barabara ya Lindi – Dar- es Salaam ambayo imeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zikiambatana na kimbunga Hidaya.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi Mha. Emil Zengo ameyasema hayo leo tarehe 5 Mei 2024 alipotembelea na kukagua uharibifu uliotokea katika eneo la Somanga - Mtama.

Amesema kuwa leo majira ya asubuhi maji yamefurika kwa wingi na kuharibu eneo la takribani mita 80 katika barabara ya Somanga – Mtama na kukata tuta la barabara hiyo eneo la Mikereng'ende umbali wa Kilomita 10 kutokea Somanga uelekeo wa Lindi.

Pia imeleta athari katika eneo la Lingaula umbali wa kilomita 12 kutokea Nangurukulu uelekeo wa Lindi


Amesema kuwa jitihada za Serikali zinaendelea kufanywa ili kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo kutokea upande wa Mkoa Pwani na kutokea Lindi.

Mha. Zengo ametoa wito kwa Wananchi na Madereva kuendelea kuwa na subira kwani Serikali kupitia TANROADS inaendelea kufanya kila linalowezekana kurejesha miundombinu ya barabara hiyo na kuwezesha Wananchi kupata huduma ya usafiri katika barabara kama kawaida.


No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

"HONGERENI JKT KWA KUENDELEZA UTALII"- DC KIBAHA

  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Nickson Simon John amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia kikosi chake cha Ruvu JKT kwa kuendelez...