Takriban watu 670 wanakadiriwa kuzikwa chini ya maporomoko makubwa ya ardhi huko Papua New Guinea, afisa wa Umoja wa Mataifa anasema.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Papua New Guinea, Serhan Aktoprak, alisema athari za maporomoko ya ardhi ya Ijumaa katika jimbo la Enga lililojitenga nchini humo ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa hapo awali.
"Kuna takriban nyumba 150 zaidi zilizozikwa," Bw Actoprak alisema.
Maeneo yaliyoathiriwa yako katika nyanda za juu za Enga, kaskazini mwa taifa la kisiwa kusini-magharibi mwa Pasifiki.
Bw Actoprak alisema waokoaji walikuwa hatarini kwa sababu "ardhi bado inateleza".
"Maji yanatiririka na hii inaleta hatari kubwa kwa kila mtu anayehusika," alisema.
Kuna karibu watu 4,000 wanaoishi katika eneo lililokumbwa na maporomoko ya ardhi.
Lakini Care Australia, shirika la misaada ya kibinadamu ambalo linasaidia katika juhudi za kutoa misaada, lilionya kuwa idadi iliyoathiriwa "inawezekana ikawa kubwa" kwa sababu ya mmiminiko wa watu wanaokimbia migogoro ya kikabila katika maeneo jirani.
Takriban watu 1,000 wamekimbia makazi yao kutokana na maafa hayo.
Lakini Care Australia, shirika la misaada ya kibinadamu ambalo linasaidia katika juhudi za kutoa misaada, lilionya kuwa idadi iliyoathiriwa "inawezekana ikawa kubwa" kwa sababu ya wimbi la watu wanaokimbia migogoro ya kikabila katika maeneo jirani.
Maporomoko ya ardhi yalitokea mwendo wa saa 03:00 kwa saa za huko siku ya Ijumaa (17:00 GMT siku ya Alhamisi), wakati kuna uwezekano mkubwa watu walikuwa wamelala.
Bw Actoprak alisema wasaidizi walikuwa wakitumia njia zozote muhimu kuokoa waathiriwa: "Watu wanatumia vitu kama majembe kuondoa miili iliyozikwa chini ya udongo."
No comments:
Post a Comment