Picha za video za CCTV zilithibitisha kile ambacho watu wengi katika tasnia ya muziki walijua kilikuwa kikisubiriwa: kipindi cha kuporomoka kwa wasanii wa hip-hop wenye ushawishi mkubwa katika historia.
Klipu za Sean "Diddy" Combs akimpiga teke mpenzi wake wa zamani Cassie Ventura - akiwa amelala bila kusonga sakafuni - ziliimarisha kuanguka kwake, licha ya kuomba msamaha baada ya kuvuja.
"Sioni njia ya yeye kurudi kwenye umaarufu wa kimuziki baada ya tukio hili," alisema Amy DuBois Barnett, mhariri mkuu wa zamani wa jarida la Ebony, ambaye ameandika kuhusu utamaduni wa hip-hop.
Sifa ya Bw Combs katika tasnia hiyo "imeangaliwa kwa muda," aliongeza Barnett. "Watu wengi walifahamu hasira yake isiyozuilika."
Diddy - ambaye awali alijulikana kama P Diddy, Puff Daddy au Puffy - ni mmoja wa wasanii maarufu zaidi na waliosifiwa zaidi wakati wote, akiwa na Tuzo tatu za Grammy na mamilioni ya mauzo ya rekodi kwa jina lake.
Kwa miaka mingi, hakuna chochote kilichoathiri kupanda kwa Diddy hadi alipopata hadhi kama msanii, mtayarishaji na mfanyabiashara. Kulikuwa na hadithi hasi katika tasnia hiyo, alisema Bi Barnett, lakini nyingi zilikaa nje ya macho ya umma.
Novemba mwaka jana, Bi Ventura alisuluhisha kesi dhidi ya Bw Combs - ambapo alimshutumu kwa ubakaji na ulanguzi wa kingono - kwa kiasi kisichojulikana. Lakini wakili wa Bw Combs alisema suluhu hiyo "kwa njia yoyote si kukiri makosa".
Watu mashuhuri waliendelea kumuunga mkono, lakini juhudi zao ziliisha pale video ya CCTV iliyopatikana na CNN ilipochapishwa wiki iliyopita.
Shambulio lililoonyeshwa kwenye picha ni la kikatili baada ya kumpiga teke Bi Ventura kama mpira wa miguu, Bw Combs, akiwa amevaa taulo tu, anaonekana akimburuta kwenye sakafu.
Video hiyo inaonekana kuwa ni mkusanyiko wa picha za uchunguzi za tarehe 5 Machi 2016, ambazo CNN ilisema zilirekodiwa katika Hoteli ya InterContinental huko Century City, Los Angeles.
Katika kesi yake, Bi Ventura alikuwa ameeleza kisa cha Machi 2016 katika hoteli hiyo, ambapo Bw Combs alidaiwa kumshambulia.
Msururu wa mashitaka mengine tangu wakati huo yaliletwa dhidi ya Bw Combs kwa unyanyasaji, unyanyasaji wa kingono na ubakaji.
Zilipowasilishwa, rapper huyo alizitaja tuhuma hizo kuwa "zinazochukiza" na kusema waathiriwa hao walikuwa wakitafuta "malipo ya haraka".
Lakini video ya kushambuliwa kwa Bi Ventura ilidhoofisha juhudi zake za kukanusha kile kilichoonekana.
Combs alikuwa kimya kwa siku mbili baada ya kuachiliwa kwake, kabla ya kutuma ujumbe wa msamaha kwenye Instagram, akikiri kuwa kweli ni yeye aliyeonekanda kwenye kanda hiyo na kuzitaja hatua zake kuwa "hazina madhara".
"Nilichukizwa wakati huo nilipofanya hivyo," alisema, "na nimechukizwa sasa."
"Nilienda na nikatafuta msaada wa kitaalamu," aliendelea. "Niliingia kwenye matibabu, kwenda kwenye kituo cha msaada wa kurekebisha tabia(rehab). Ilinibidi kumuomba Mungu huruma na neema yake. Samahani sana."
Combs hakumtaja Cassie Ventura katika msamaha wake, na wanasheria wake walimjibu, waakisema: "Kauli ya hivi karibuni ya Combs inamhusu yeye mwenyewe kuliko watu wengi ambao amewaumiza."
Msamaha huo "ulichelewa sana," alisema Camron Dowlatshahi, wakili wa masuala ya burudani huko Los Angeles. "Inaonyesha kutoona mbali kwa Diddy, akidhani hatawajibishwa na kwamba ana pesa za kutosha kushughulikia kila kitu."
Barnett, ambaye ameandika kuhusu unyanyasaji wa wanawake katika tasnia ya rap, alielezea kauli hiyo kama "msamaha usioshauriwa zaidi kuwahi kutokea".
Alisema ulitoka kwenye "kitabu maarufu cha playman : kanusha, kanusha, kanusha . Ukipatikana na hatia . Omba msamaha, kisha zungumza kuhusu kwenda kutibiwa."
"Hakuna anayeuchukulia msamaha wake kwa uzito, hasa kwa sababu hapo awali alimshutumu Cassie na wengine kuwa watu waliotafuta mali. Hiyo ilikasirisha watu wengi katika tasnia ya muziki."
Picha za angani zinaonyesha uvamizi wa mali za Sean 'Diddy' Combs. |
Picha za familia pamoja na binti zake zilizochapishwa kwenye akaunti ya Instagram ya Bw Combs ni tofauti kabisa na picha zake akitekeleza shambulio la kikatili.
Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Los Angeles ilisema Ijumaa kwamba haitaweza kuleta mashtaka kutokana na sheria ya vikwazo vya shambulio.
Katika muziki wake, Diddy mara nyingi amekuwa akitegemea ushirikiano na nyota wengine wa maarufu (A-list). Albamu yake ya mwisho ilishirikisha Mary J Blige, The Weekend, 21 Savage, John Legend. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hawezi kuunda tena matoleo kama haya sasa.
Lakini iwa kutakuwa na athari kwa idadi kubwa ya wasikilizaji wake hilo si wazi. Kampuni ya Fitness Peloton imepiga marufuku muziki wake kwenye orodha za kucheza za mazoezi tayari, kulingana na TMZ, lakini kampuni zingine bado hazijatoa maoni.
R Kelly anaendelea kupata mamilioni ya wasikilizaji wa kila mwezi kwenye Spotify, licha ya kukutwa na hatia ya kuwanyanyasa watoto kingono.
Wakati huo huo, Kanye West alipata kiwango cha juu zaidi cha cha wasikilizaji wa muziki wake wa kila mwezi mwaka jana, licha ya kuachwa na chapa kwa kutoa maoni ya chuki.
Wasanii waliopita na nyota wa Diddy kwenye zulia la Hollywood Walk of Fame wiki hii walitafakari video hiyo ilimaanisha nini kwa mashabiki wa rapper huyo.
"Ni mwisho wa kazi. Sijui atarudi vipi kutoka kwa hii," alisema Mar Anthony, mwenyeji wa Los Angeles. "Nilikuwa shabiki wakati nikiwa mtoto, nikisikiliza -Every Breath You Take (I'll Be Missing You) Lakini alichokifanya na muziki, ni vitu viwili tofauti.
"Ni kitu sawa na Michael Jackson," alisema, akiashiria nyota mwingine wa Walk of Fame - katika kumbukumbu ya wazi ya madai ya unyanyasaji wa watoto yaliyotolewa dhidi ya nyota huyo.
Diddy "hakika anastahili kile kinachomtokea ", alisema Prince Laurenz Hamlin, ambaye alikuwa akitembelea LA. "Lakini bado amejijengea historia katika tasnia ya muziki. Nafikiri itabidi watu watenganishe sanaa na msanii."
Haijulikani ni nani anayemshauri Sean Combs kwa sasa. Kampuni ya mawakili ambayo hapo awali ilitoa tangazo la kukanusha shutuma zake kwa niaba yake imesema haimuwakilishi tena.
Licha ya mashtaka ya madai hakujawa na mashtaka ya jinai yaliyowasilishwa dhidi yake.
Lakini uchunguzi unaoendelea wa polisi bila shaka utakuwa na uzito kwa msanii huyo wa rap.
"Wizara ya Usalama wa Ndani ilihusika [katika uvamizi huo]," alisema Bw Dowlatshahi. "Ukweli huo pekee unaonyesha ukali wa kile kinachoendelea hapa."
No comments:
Post a Comment