Na Okuly Julius , Dodoma
Dkt.Tax amesema Kati ya fedha hizo Shilingi Trilioni
3.008 sawa na asilimia 90.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 317.41 sawa
na asilimia 9.5 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Dkt. Tax ameanisha shughuIi
zinazokusudiwa
kutekeIezwa katika Mwaka wa Fedha 2024/25 zitazingatia
maeneo ya kipaumbeIe yafuatayo:
Moja ,KuendeIea kuIiimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa,
mafunzo na mazoezi, pamoja na rasiIimaIi watu;
Mbili, KuendeIea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi wa
Jeshi ikiwemo masIahi, huduma bora za afya na makazi;
Tatu, Kuimarisha miundombinu mbaIimbaIi katikamaeneo ya Jeshi;
Nne , Kuimarisha mashirika na taasisi katika Sekta ya UIinzi;
Tano, KuendeIea kushiriki katika ujenzi na uIinzi wa miradi ya
kimkakati kwa masIahi mapana ya Taifa;
Sita , KuendeIea kuimarisha uwezo wa Jeshi Ia Kujenga Taifa
kwa kuboresha miundombinu iIi Iiweze kuchukua vijana
wengi zaidi watakaopata mafunzo ya uzaIendo,
ukakamavu, umoja wa kitaifa, na stadi za kazi kwa vijana
wa kundi Ia Iazima na wakujitoIea;
Kufanya tathmini ya haIi iIivyo ya mafunzo ya JKT na
kuandaa Mpango Mkakati utakaoainisha mahitaji, bajeti na
muda wa utekeIezaji, kwa Iengo Ia kuweza kuchukua vijana
wote wanaostahiIi kupata mafunzo ya JKT kwa kundi Ia
Iazima;
Saba, Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja
wa Afrika (AU), Jumuiya za Kikanda, na nchi mbaIimbaIi
katika nyanja za kijeshi na kiuIinzi na hivyo kuimarisha
DipIomasia ya UIinzi; na
Nane, KuendeIea kushirikiana na MamIaka za Kiraia katika
kukabiIiana na majanga na dharura inapohitajika.
Wakati huo huo Waziri Tax amesema Wizara kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) imeendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, kuwajengea uzalendo, umoja wa kitaifa, na stadi za kazi. Idadi ya waliopatiwa mafunzo imeongezeka kutoka 26,000 katika mwaka wa fedha 2022/23 hadi kufikia 52,119 katika mwaka wa fedha 2023/24.
Ameongeza kuwa kati ya hao waliopewa mafunzo, wavulana ni 31,256 na wasichana ni 20,863.
“Aidha, vijana 12,000 wa kujitolea wanaendelea kupatiwa mafunzo katika makambi mbalimbali ya JKT,” alisema.
Dkt. Tax ametoa rai kwa wananchi kutovamia maeneo ya Jeshi, kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa maisha yao kutokana na shughuli za kijeshi zinazofanyika katika maeneo hayo, ikiwemo mafunzo na mazoezi mbalimbali yanayotumia risasi za moto, milipuko, na zana zenye mionzi.
Amesema kufanya uvamizi katika maeneo hayo ni kuhatarisha usalama wa Taifa na kukwamisha shughuli muhimu za kuliweka tayari Jeshi kukabiliana na matishio yoyote yanayoweza kujitokeza.
“JWTZ inamiliki maeneo ya kimkakati katika mikoa mbalimbali nchini ambayo yametengwa maalum kwa matumizi ya kijeshi,” alisema.
No comments:
Post a Comment