Na Saida Issa,Dodoma
SERIKALI imesema kuwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Makofia – Mlandizi – Mzenga – Maneromango yenye urefu wa kilometa 100 umefanyika na kukamilika.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Viti Maalum Subira Mgalu alipouliza Je, lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Makofia – Mlandizi – Mzenga hadi Maneromango kwa kiwango cha lami.
"Katika mwaka wa fedha 2023/24, Shilingi bilioni 2.5 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mlandizi – Ruvu SGR (km 23) ikihusisha kilometa 15 za barabara ya Makofia – Mlandizi – Mzenga – Maneromango kipande cha kutoka Mlandizi – Ruvu Junction na Roundabout ya makutano ya Mlandizi,"alisema.
Alisema kuwa kwa sasa taratibu za manunuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa Mlandizi – Ruvu SGR (km 23) zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Juni, 2024,Kwa sehemu iliyobaki Serikali inaendelea kutafuata fedha za kuendelea na ujenzi.
No comments:
Post a Comment