DKT. RWEZIMULA AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA KIMATAIFA LA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU UDOM. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 18, 2024

DKT. RWEZIMULA AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA KIMATAIFA LA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU UDOM.


Na Carlos Claudio,Dodoma.


Kongamano la kwanza kimataifa la sayansi, teknolojia na ubunifu limefunguliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM lenye dhamira ya maendeleo ya sasa katika sayansi, teknolojia na uvumbuzi yaweze kuleta faida endelevu katika viwanda na jamii.


Akizungumza leo Juni 18, 2024 Naibu katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amesema vyuo vikuu vimefanya kazi ya kufanya tafiti tofauti na kutangaza matokeo hayo kwa jamii yanayosaidia katika usuluhisho wa changamoto.


Amesema kwenye sayansi, ubunifu na teknolojia kuna mambo mapya yanayotokea duniani na Chuo Kikuu Cha Dodoma hakipo nyuma kuendana na mabadiliko hayo.


“Leo wanaonyesha matokeo ya tafiti walizozifanya na jinsi gani wamechangia kwenye jamii ya wasomi lakini Chuo Kikuu cha Dodoma kina mchango mkubwa sana kwa serikali yetu,”


“Kwaio nimefika leo kuangalia wanachokifanya, wana maonyesho mazuri, kuna teknolojia wanafanya wamebuni na wanafunzi wanashiriki vizuri na mpango wao mpaka mwaka 2026 kiwe ni chuo namba 1 Tanzania ambacho kitakuwa kimetoa machapisho mengi.” amesema Rwezimula.


Aidha amesema tafiti hizo zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma zimekuwa msaada kwa serikali katika kupata majawabu ambayo yanarahisisha ufanyaji wa kazi.


Kwa upande wa makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma profesa Lughano Kusiluka amesema mkutano huo wa kwanza umetayarishwa kwaajili ya kujadili mambo ya sayansi, teknolojia na ubunifu  huku ukihudhuriwa na wanasayansi wabunifu kutoka ndani na nje ya nchi.


Kusiluka amesema chuo Kikuu cha Dodoma kina wataalamu katika idara tofauti ikiwemo mambo ya mabadiliko ya tabia nchi, jografia pamoja na kitengo kinachofundisha namna ya kupambana na majanga pamoja na wahandisi wa mambo ya mazingira.


Kusiluka ameongeza kuwa “Hakuna mahali ambapo UDOM sasahivi wataalamu wakakusanyika na kukosekana, nadhani serikali ina mpango mzuri sana kuvihusisha vyuo vikuu kwasababu uwekezaji kwenye vyuo vikuu vyovyote lengo lake ni kutatua changamoto za jamii.”


Nae raisi wa ndaki ya sayansi asilia na hisabati Saidi Vuai amesema mkutano huo ni zao endelezi la wiki ya CNMS lenye lengo la kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha umahili wao kupitia mafunzo wanayoyapata.


Amesema lengo la ndaki hiyo ya sayansi asili na hisabati ni kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa na sifa ya kuajirika, uwezo wa kujiajiri pamoja na uwezo wa kuongeza thamani kwa kazi wanazozifanya kwenye jamii.


“Tafiti hizi zinatakiwa baada ya kufanywa na kupata matokeo yake ndio ambazo zinaweza zikatoa taarifa kwa wakufunzi namna ya kufundisha  lakini pia kutoa matokeo ambayo yanaweza kusaidia kufanya kazinza huduma kwa jamii.” amesema Vuai.











No comments:

Post a Comment