PATO LA TAIFA LAONGEZEKA KWA 5.1% - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 18, 2024

PATO LA TAIFA LAONGEZEKA KWA 5.1%

 


Na Saida Issa, Dodoma 


IMEELEZWA kuwa katika kipindi cha mwaka 2023, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 5.1 ikilinganishwa na ukuaji wa

asilimia 4.7 mwaka 2022. 


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya bajeti Oran Njeza alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati kuhusu tathmini ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2023,Mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2023/24 utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2023/24 pamoja na mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25. 


Alisema kuwa Ukuaji huo umekaribia makadirio ya IMF ya asilimia 5.2,Katika mwaka 2023, thamani halisi ya Pato la Taifa ilifikia shilingi trilioni 148.399 ikilinganishwa na shilingi trilioni 141.873 ya mwaka 2022.


"Hata hivyo, ukuaji huo wa uchumi wa Taifa haujaweza kufikia lengo la asilimia

5.5 lililokuwa limewekwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa

Mwaka 2023/24, 


Ukuaji huu unadhihirisha kwamba Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amedhamiria kunaendelea kuimarisha uchumi ili

kufikia malengo ya ukuaji wa asilimia 5.5 ambao Serikali imejiwekea katika kipindi cha muda wa kati,"alisema.


Kadhalika alisema kuwa Kamati imebaini kushuka kwa mfumuko wa bei nchini kumetokana na kupungua kwa bei ya nafaka hususan ngano, mchele, mahindi na mtama pamoja na utekelezaji wa sera ya fedha ya kupunguza ukwasi na

kupungua kwa bei za bidhaa katika soko la Kimataifa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023/24.


"Kamati inaishauri Serikali

kupitia Benki Kuu ya Tanzania na Wizara ya Fedha kuweka mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya jinsi ya kukabiliana na mfumuko wa bei unaoingizwa nchini (Imported Inflation) ili kutoathiri uchumi wa Taifa,Vilevile Serikali iweze kuwianisha kati ya mfumuko wa bei na ukuaji wa uchumi,"alisema.


kwa mujibu wa Kanuni ya 124(8) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Februari, 2023 na kwa kuzingatia kifungu

cha 9 (1) na (2) cha Sheria ya Bajeti Sura ya 439, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Tathmini ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2023, Mpango wa

Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2023/24, Utekelezaji wa Bajeti ya

Serikali kwa mwaka 2023/24 pamoja na Mapendekezo ya Mpango na

Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25.

No comments:

Post a Comment