Na Saida Issa, Dodoma
MWENYEKITI wa kamati ya bunge ya bajeti Oran Njenza amesema kuwa Kamati inashauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuwashirikisha wadau mapema kabla ya kuwasilisha mapendekezo ya Sheria katika Jumuiya.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya maoni ya kamati kuhusu muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2024.
"Ushirikishwaji wa Wadau kwenye Mabadiliko ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004 Mheshimiwa Spika,Kamati imebaini kwamba kuna ushirikishwaji hafifu wa wadau katika mabadiliko ya Sheria hiyo na hivyo wadau kushindwa kuwasilisha kwa wakati changamoto na maoni ya kikodi za Sheria hiyo,"amesema.
Kadhalika amesema kuwa Serikali kufanya Tathmini ya Hatua za Kikodi inazozichukua kila mwaka kwa kodi za ndani na Kodi ya Ushuru wa Forodha wa Afrika Mashariki.
"Kamati imebaini kwamba Serikali haina
utaratibu wa kufanya tathmini ya matokeo ya hatua za kikodi
zinazochukuliwa kila mwaka ili kuangalia endapo zina manufaa hasi au chanya kwa uchumi na uzalishaji viwandani,
Hivyo,Kamati inaitaka Serikali kila mwaka kufanya Tathmini ya
kina ya athari hasi na chanya zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa mapendekezo ya mwaka uliopita,"amesema.
Pia amesisitiza Kufanya Mabadiliko ya ukusanyaji wa Ada na Tozo mbalimbali bila kuwa na mifumo ya ukusanyaji, Serikali imekuwa ikifanya mabadiliko ya ukusanyaji wa tozo na ada mbalimbali bila kuandaa mifumo ya ukusanyaji.
"Hatua hii imekuwa na athari katika makusanyo kwa sababu kwa baadhi ya tozo zinachelewa kukusanywa hadi
miezi 7 baada ya mwaka wa fedha kuanza,
Kadhalila alisema kuwa Kamati inaishauri Serikali kabla ya kufanya mabadiliko yoyote kuandaa
mifumo ya ukusanyaji kwanza,"amesema.
No comments:
Post a Comment