MSONDE:TUMIENI MFUMO KUSHUGHULIKIA UHAMISHO WA WATUMISHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 19, 2024

MSONDE:TUMIENI MFUMO KUSHUGHULIKIA UHAMISHO WA WATUMISHI



OR-TAMISEMI


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka watendaji wa Hamshauri nchini kushughulikia uhamisho wa walimu na watumishi wengine kwa kutumia mfumo uliowekwa ili kuondoa sitofahamu zinazojitokeza.


Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi cha majumuisho ya ziara yake katika mkoa wa Tabora kilichowakutanisha walimu wakuu wa shule,Maofisa Elimu na wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa  huo kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Mihayo Manispaa ya Tabora.


“Siku zote kuwa makini kuona kwenye mfumo tunapitisha nini kwasababu watu wameomba uhamisho ni lazima tuwapitishie ili mwenye mamlaka ya kuidhinisha uhamisho akiona haistahili yeye atakataa lakini sisi tuwapitishie kulingana na maombi yao, ” amesema

Dkt. Msonde amesisitiza kuwa endapo mkurugenzi atakuwa amebanwa na shughuli zingine na kushindwa kuingia kwenye mfumo anapaswa kukasimu mamlaka kwa mtu mwingine ili kuhakikisha maombi hayakai kwa muda mrefu na kuwaacha watumishi wakilalamika.


Akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora, Grace Quintine ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo ameahidi kufanyia kazi maelekezo hayo na kuyasimamia ili kuwe na ufanisi katika sekta ya Elimu katika mkoani humo.

No comments:

Post a Comment