SERIKALI IMEWEKA KIPAUMBELE KUBORESHA NA KUKAMILISHA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YA KIUTAWALA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 3, 2024

SERIKALI IMEWEKA KIPAUMBELE KUBORESHA NA KUKAMILISHA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YA KIUTAWALA

 


Na Saida Issa,Dodoma

SERIKALI imesema kuwa inatambua mahitaji na umuhimu wa kuanzisha maeneo ya kiutawala ili kusogeza huduma karibu na wananchi. 


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Festo Dugange alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Serikali itapandisha hadhi ya Mji Mdogo wa Mbalizi kuwa Halmashauri ya Mji wa Mbalizi. 


Amesema kuwa uanzishaji wa maeneo ya utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na (Mamlaka za Miji) Sura 288 pamoja na Mwongozo wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa Mwaka 2014.


"Mheshimiwa Spika, Kwa sasa serikali imeweka kipaumbele katika kuboresha na kukamilisha miundombinu kwenye maeneo yakiutawala yaliyopo,


ili yaweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi na baadae kuendelea na maeneo mengine kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyoainishwa ikiwemo mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi,"amesema Naibu Dugange .

No comments:

Post a Comment