SERIKALI YASEMA UANZISHWAJI WA MAENEO YA UTAWALA NI KWA MUJIBU WA SHERIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 20, 2024

SERIKALI YASEMA UANZISHWAJI WA MAENEO YA UTAWALA NI KWA MUJIBU WA SHERIA


Na Saida Issa, Dodoma 

SERIKALI imesema kuwa uanzishaji wa maeneo ya utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na (Mamlaka za Miji) Sura 288 pamoja na Mwongozo wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa Mwaka 2014.


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais(TAMISEMI)Zainab Katimba alipokuwa kuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Serikali itarekebisha mipaka ya Vijiji vya Kata ya Utengule na Usongwe ikiwemo Kijiji cha Mbalizi ambacho hakiungani kabisa na Vijiji vingine. 


"Kwa kuzingatia sheria hizi na mwongozo uliopo, utaratibu wa uanzishaji au mabadiliko ya mipaka ya vijiji inapaswa kuanza kujadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji, Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC),


Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) na Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ambayo huwasilisha mapendekezo hayo Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupitia Katibu Tawala Mkoa,"alisema. 


Alisema kuwa ni vema Halmashauri na Mkoa kufuata taratibu hizo na ombi hilo liwasilishwe Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupitia Katibu Tawala Mkoa kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment