Na Jasmine shamwepu,Dodoma.
Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa kushirikia na Wizara ya Maji kimeanza kutekeleza mradi wa ustaimilivu wa mabadiliko tabianchi katika nyanja za kitropiki.
Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu katika maeneo yenye shida ya maji ukiwa na lengo la kuangalia namna ya kukabiliana na mabadiliko tabianchi katika maeneo yanapata mvua chini milimita 500 kwa mwaka.
Mkurugenzi katika kurugenzi ya Uzamili, utafiti uhaulishaji wa teknolojia na Ushauri wa kitaalam ambaye ni Kiongozi wa utafiti wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na ustahimilivu katoka nyanda kavu za kitropiki Profesa Japheth Kashaigili amebainisha jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao cha wadau kutoka sekta binafsi pamoja na wananchi.
Amesema mradi huo unalenga kuangalia namna bora ambavyo itasaidia kukabiliana na mabadiliko tabianchi katika maeneo ya kitropiki yenye shida ya maji juu ya ardhi.
"Mradi huu utatelezwa hapa Dodoma ikiwa ni moja ya eneo ambalo linachangamoto ya upagikanaji wa maji kwani Dodoma pia ni mkoa ambao unategemea chanzo cha maji chini ya ardhi katika bonde la Mzakwe"amesema
Amesema kutoka na mahitaji ya maji kuongezeka ipo haja ya kufahamu mwenendo wa upatikanaji wa maji chini ya ardhi.
"Dodoma inategemea maji chini ya ardhi kupitia chanzo cha Mzakwe kilichopo bonde la Makutupora kwa asilimia 60 hivyo lipo hitajio la kujua mwendo wa maji katika chanzo hicho.
Amesema kutokana na ongezeko la mahitaji ya maji katika mkoa wa Dodoma ikiwemo shughuli za kibinadamu inatupaswa sisi wataalam kujua mwenendo wa maji chini ya ardhi na mahitaji yaliyopo ili tuweze kujipanga.
Amesema mradi huo ambao ulizinduliwa mwaka jana unatekelezwa kupitia maabara za mabadiliko ambazo zinapima kiasi cha maji kinacho nywea kwenye udogo.
Aidha amesema kutoka na mipango inayofanywa na serikali kupitia wizara ya maji wao kama wataalam wa vyuo Vikuu wameona ipo haja ya kushiriki kutatua changamogo ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo ya kitropiki.
"Hivi sasa kuna visima vingi vinachimbwa kwenye nyumba, hoteli hivyo ni muhimu ni sana kufaahamu mwenendo wa maji chini ya ardhi na mahusiano ya ongezeko la matumizi ili baadaye tuweze kuwa na mipango mizuri tusije tukashanga kikatokea kitu kingine ambacho tulikuwa bado hatujajiandaa"amesema
Kashaigili amesema wanahitaji kuujua mfumo mzima wa maji na shughuli za kibinadamu zinazo endelea na wakiweza kufanya hivyo inamaana wanaweza kuona kitu gani kifanyike kuweza kusaidia uzalishaji wa maji kwenye maeneo mbalimbali lakini.pia kuwa na angalizo twende mpaka hatua gani isije ikawa ni changamoto.
"Kwahiyo ni utafiti ambao ni miaka.mitatu na nusu sasa tunakwenda miaka miwili na nusu baada ya kwenda mwaka wa kwanza katika.kuangalia namna ya kuleta suluhu mbalimbali katika suala hili na kama nilivyosema tunafanya kwa kushirikiana na wadau ni watu wa msingi sana kila kinachopatikana lazima tujadiliane na kuhakikisha kwamba matokeo yanayopatikana yatoa suluhu ya uhakika"amesema
Angalia wa maji chini ya ardhi na shughuli zinazofanyika ili baadae kuja na mipango ambayo itasaidia shughuli zinazofanyika sehemu fulani zikaathiri upatikanaji wa maji"alisema
Hata hivyo amesema kuna stadi nyingi zimefanyika kuhusu vyanzo vya maji ambavyo vipo kuna vitoa maji hadj muda gani lakini wao wamekuwa kuja na utafiti huo ili kuleta majibu
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokoinecha kilimo Taaluma,Utafiti na Utaalam Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) Prof. Maulid Mwatawala, amesema Dodoma ni sehemu ya nyanda kavu yenye changamoto ya upatikanaji wa maji hivyo umuhimu wa kuangalia maji yaliyo chini na kuyatunza na
"Kuyasamba kwa usawa katika jinsia zote uwe endelevu lakini pia wa uhakika.
"Kwahiyo.kundi hilo limekaa hapa kuangalia nini utakua mchango wa maji ambayo yapo ardhini katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji hapa Dodoma" amesema
Amesema athari za mabadiliko tabianchi ni nyingi maji kupungua na kutokuwepo lakini kwa sasa tunaangalia zaidi nini kimetupeleka hapa wadau walipo hapa wameona masuala mbalimbali yanayopelekea kupoteza vyanzo vya maji ni pamoja na.kuwa na makundi makubwa ya mifugo,vibali holela vya uchimbaji wa mchanga,lakini uvunaji mvua kwa sababu hili eneo la ukame.
Wadau wameona ili tuweze kwenda mbele lazima tutunze vyanzo vya maji kwa upandaji na utunzaji wa miti,pia kuna suala la kisera kwamba maji ni suala la mtambuka watu wa kilimo wanatumia,mifugo wanatumia,nishati wanatumia Sera inaweza ikawa mtambuka lakini bado hatua sheria inayo wakutanisha wadau wote kuamua kwa pamoja.
Mfano kuna sheria inakataza ujenzi wa makazi katika mitaa kadhaa lakini mtu wa kibali anaweza toa kibali bila kufuata sheria ile na akanenga maeneo yaliyo karibu na chanzo cha maji kwa hiyo inahitajika Sera ambayo itaunganisha watu wote.
No comments:
Post a Comment