TANROADS NA ZANROADS WAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 11, 2024

TANROADS NA ZANROADS WAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO.


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS) katika kutekeleza mpango kazi wao wa kipindi cha mwaka mmoja, ambao utekelezaji huo utaanza kutumika rasmi  mwaka wa fedha 2024/25, wameweza kufanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.


Lengo la kutembelea na kukagua mradi huo ni kujifunza utaalam na masuala ya uendeshaji na uongozi hasa kuwa na wataalamu wa kutosha kuweza kusimamia miradi bila kuwa na uharibifu.


Akizungumza muda mfupi baada ya kufanyika kwa kikao cha kipitisha rasimu ya mpango kazi wa mwaka 2024/25 uliofanywa na Kamati ya Wataalam na Kamati ya Uongozi  leo Juni 10, 2024, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya ZANROADS, Msanifu Majengo Yasser de Costa amesema wamefarijika kuona maendeleo yaliyofikia pamoja na kukutana na mshauri elekezi wa Beza Consulting Engineering aliyetoa maelezo pamoja na kukutana na wakandarasi wawili BCEG na Sinohydro Corporation Ltd katika mradi huo wa uwanja wa ndege wa Msalato.


“Kwa maoni yetu na mtizamo kwanza tunawapongeza wahusika wote watendaji katika ujenzi huu kwa hatua waliyofikia lakini la pili napenda kuchukua fursa hii tena kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dtk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa msimamo na uzito wa kujenga jengo kama hili la uwanja wa ndege,”


De Costa ameongeza kuwa,“ sote tunaelewa kwamba uwanja wa ndege una umuhimu sana katika maendeleo ya nchi na kaa wale ambao wana bahari bandari pia inasaidia katika kuendeleza nchi, hizi sehemu mbili bandari na uwanja wa ndege ndio viingilio vya wananchi, watalii pamoja na wazalendo.”


Amesema kupitia ziara hiyo wameweza kuuliza na kufahamu kuwa wakandarasi wataweza kukamilisha jengo hilo pamoja na miundombinu kwa muda ambao wamepangiwa mwezi wa Novemba 2025 na mtizamo wake unaona muda ni mfupi hivyo wameweza kutoa ushauri na mawazo kwa wakandarasi kujipanga tena kwa kuzingatia ratiba zao ikiwezekana kufanya kazi usiku na mchana ili jengo liweze kukamilika kabla ya muda na ikiwezekana kabla ya uchaguzi mkuu.


Aidha de Costa ameeleza mmoja ya faida ya kumaliza ujenzi kabla ya uchaguzi ni fursa kwa viongozi kufungua pamoja na kuzindua jengo ili wananchi waweze kutumia.


Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalato Mha. Mahona Limbe kutoka TANROADS amesema katika utekelezaji wa mradi huo wana wakandarasi wawili ambao mmoja anahusika na ujenzi wa miundombinu ya barabara ambaye ni Sinohydro Corporation Ltd pamoja na mkandarasi wa pili anayehusika na miundombinu ya majengo.


Amesema mikataba yote kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo ni miaka mitatu na mkandarasi wa miundombinu ya barabara alianza kazi Aprili 2022 na matarajio yao ifikapo Aprili 2025 mradi huo wa miundombinu ya barabara utakuwa umekamilika.


“Gharama za ujenzi wa miundombinu ya barabara ni bilioni 165 za kitanzania na mkandarasi wa miundombinu ya majengo yeye alianza kazi mwezi Novemba 2022 na yeye tunatarajia ifikapo mwaka 2025 mwezi Novemba ataweza kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya majengo,”


“Gharama za miundombinu ya majengo ni bilioni 194 za kitanzania, kupitia mradi huu tunatarajia utaweza kuhudumia watu milioni 1 na nusu kwa mwaka hivyo tunajitahidi kumuhimiza mkandarasi ili aweze kumaliza kwa wakati.” amesema Limbe.


Limbe ameeleza kuwa mkandarasi wa barabara amefikia asilimia 64 na mkandarasi wa majengo amefikia asilimia 27 wakiwa wanapishana kutokana na utofauti wa kuanza kazi.











No comments:

Post a Comment