TANROADS NA ZANROADS WAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA BARABARA ZA MZUNGUKO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 11, 2024

TANROADS NA ZANROADS WAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA BARABARA ZA MZUNGUKO.


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Zanzibar (ZANROADS) katika kutekeleza mpangokazi wao wa kipindi cha mwaka mmoja, ambao utekelezaji huo utaanza kutumika rasmi  mwaka wa fedha 2024/25, wameweza kugfanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.


Lengo la kutembelea na kukagua mradi huo ni kujifunza utaalam na masuala ya uendeshaji na uongozi hasa kuwa na wataalamu wa kutosha kuweza kusimamia miradi bila kuwa na uharibifu.


Akizungumza muda mfupi baada ya kufanyika kwa kikao cha kipitisha rasimu ya mpango kazi wa mwaka 2024/25 uliofanywa na Kamati ya Wataalam na Kamati ya Uongozi  leo Juni 10, 2024, Mtendaji Mkuu wa ZANROADS, Mha. Cosmas Masolwa amesema ujenzi wa barabara za mzunguko hasa daraja la Ihumwa ni mmoja ya miundombinu mikubwa inayojengwa kwenye barabara hiyo ya mzunguko wa mji wa Dodoma yenye jumla ya kilomita 112.3.


Amesema mradi unaendelea vizuri chini ya mshauri muelekezi Inter Consult pamoja na kupongeza serikali kwa kufadhili huo mradi kushirikiana na benki ya maendeleo Afrika.


“Ni mradi ambao utatatua changamoto ya msongamanonwa magari katika mji wa Dodoma, Mkandarasi kwa muujobu wa taarifa amefikia asilimia 71 ya kazi zinazoonekana na anaendelea, kwa maelezo anatakiwa amalize mwezi Disemba mwaka huu,”


“Pamoja na hilo kazi ngingi ameshafanya, cha msisitizo zaidi TANROADS kuhakikisha kwamba nao wanafuatilia kwasababu Disemba sio mbali na kwanuzoefu wangu mdogo ninaona bado kazi ni kubwa na kuna uwezekano wa kuongezaa muda hapa.” amesema  Masolwa.


Mha. Masolwa ameongeza kuwa mradi huo utasaidia katika kuongeza uchumi kwa wananchi na nchi kwa ujumla kwani ni mkakati wa miaka mingi iliyopita.


Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa barabara za mzunguko Mha. Issa Mjema amesema mradi huo umeanza Septemba  8, 2021 na unategemewa kuisha mnamo Disemba 7, 2024.


Mha Mjema amesifu jitihada za ujenzi wa barabara hiyo unayoanzia Nala ikivuka barabara ya Singida kuelekea Veyula ambayo ni barabara ya Arusha na kisha kuelekea Mtumba hadi Ihumwa kwa urefu wa kilomita 52.3.








No comments:

Post a Comment