TBS YATOA ELIMU YA UDHIBITI BORA WA BIDHAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA UTUMISHI WA UMMA 2024. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 20, 2024

TBS YATOA ELIMU YA UDHIBITI BORA WA BIDHAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA UTUMISHI WA UMMA 2024.



Na Carlos Claudio, Dodoma.


 Shirika la viwango Tanzania TBS limejikita katika kutoa huduma na elimu kupitia mifumo ya kidijitali nchini, kuelekea wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma 2024 imeweza kufikia jamii kupitia kanda zake 7 zinazotoa huduma kwa wananchi.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20, 2024 jijini Dodoma, mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala Viola Masako amesema hao kama shirika wapo hapo kuonyesha huduma zake kwa wananchi ikiwa kazi kubwa kuhakikisha wana andaa viwango na kudhibiti viwango vinavyotumika kwa wananchi.


Amesema wanamajukumu mengi ikiwa kupima bidhaa, kuangalia ubora wake, kukagua bidhaa za ndani ya nchi pamoja na zile zinazosafirishwa kwa matumizi ya ndani ya nchi ambazo ubora wake haujadhibitishwa zilipotoka


“Pamoja na hayo tunafanya kazi pia kwa wataalamu wetu wanatengeneza bidhaa mbali mbali, wanataka kusafirisha nje ya nchi kama shirika pia huwa tunawapa msaada wa jinsi watakavyoweza kutimiza vigezo na kuweza kusafirisha bidhaa zao nje ya nchi,”


“Kwa mwaka huu tunashukuru elimu hii tunayoitoa imepokelewa na muutikio umekuwa mkubwa watu wengi wamekuja kuangalia nini tunafanya katika huduma hii ambayo tunayoitoa kama shirika," amesema Masako.


Aidha amesema kuwa TBS imepata maudhurio mazuri pamoja na kutoa elimu kwa wananchi pamoja na watumishi wa serikali ambao wamekuja Dodoma kushiriki maonyesho hayo katika viwanja vya Chinangali.


Sambamba na hayo Masako ameeleza kuwa maonyesho ya mwaka 2024 wageni ambao wamewapokea wengi wao walikuwa na dhamira ya kufahamu masuala ya udhibiti bora ambao wataalamu wameweza kuwafahamisha lakini pia kwa namba gani wanaweza kuwafikia TBS.


Amesema kama shirika wana Kanda 7 ikiwemo Kanda ya Mashariki iliyopp Dar Es Salaam, Kanda ya Kaskazini iliyopo Arusha, Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara, Kanda ya Magharibi iliyopo Kigoma , Kanda ya Nyanda za Juu Kusini iliyopo Mbeya, Kanda ya kati iliyopo Dodoma pamoja na kanda ya Ziwa inayopatikana Mwanza.


Masako ameongeza kuwa,“ Hii mikoa yote inahudumia mikoa yote ya Tanzania, hivyo ni rahisi sana kwenda kufwatilia, tunatoa matangazo mbali mbali kwenye vyombo vya habari na hivyo tuna amini kabisa kwa kufanya hivyo wataweza kupata huduma zetu kiurahisi.”


Pia amesema TBS imekuwa ikitoa huduma zao kupitia namba ya simu ya huduma kwa wateja pamoja na tovuti yao ya www.tbs.go.tz katika kuhudumia pamoja na kutafua changamoto za wananchi.


Aidha ameongeza kuwa TBS katika kuangalia usalama wa raia inasisitiza jamii kutumia bidhaa zilizothibitishwa na shirika la viwango Tanzania itakayowasaidia na kuokoa maisha yao.


Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanaendelea  katika Viwanja vya Chinangali  jijini Dodoma ambayo yalianza Juni 16,2024 na yanatarajia kufungwa Juni 23,Mwaka huu.







No comments:

Post a Comment