DC SAME ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA MKOA KILIMANJARO DKT. TIXON NZUNDA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 20, 2024

DC SAME ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA MKOA KILIMANJARO DKT. TIXON NZUNDA.


Na Ashrack Miraji, Same.


Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Kasilda Mgeni akitoa heshima ya mwisho kwa aliyekua Katibu tawala wa mkoa huo Dkt.Tixon Nzunda, nyumbani kwake manispaa ya Moshi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Dar Es Salaam na baadae Mkoani Songwe kwenye shughuli za Maziko.


"wananchi wa wilaya ya Same tutaendelea kukumbuka busara na hekima zako kwenye uongozi, ni ngumu kuamini lakini kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu kuwa, "mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi" (Ayub14:1-2) hatuna namna nyingine zaidi ya kukuombea kwenye maisha mengine huko mbele za Mungu".


Nzuda alifariki dunia pamoja na dereva wake Alphonce Edson kwenye ajali Juni 18, 2024 wilayani Hai alipokua kwenye majukumu yake ya kikazi.









No comments:

Post a Comment