VIJANA KUPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPATA MIKOPO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 4, 2024

VIJANA KUPATIWA MAFUNZO KABLA YA KUPATA MIKOPO


Na Saida Issa,Dodoma


SERIKALI imesema kuwa ili kuwaandaa vijana kabla ya kupatiwa mikopo, Vijana wamekuwa wakipatiwa mafuzo ya Ujasiriamali, Uanzishaji wa Miradi, Usimamizi na Uendelezaji na Urasimishaji. 


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,vijana na wenye ulemavu Patrobasi Katambi alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Moshi Vijijini Prof.Patrick Ndakidemi alipouliza Je, Serikali inatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kiasi gani kwa vijana kabla hawajapatiwa huduma za Mikopo toka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.


Naibu katambi amesema kuwa pia vijana wanaunganishwa na huduma wezeshi kupitia Taasisi za fedha na Benki, Mamlaka za Kodi, Mamlaka za uendelezaji viwanda vidogo vidogo (SIDO); Huduma za uthibiti usalama na viwango (TBS, OSHA na TMDA) na huduma za hifadhi ya jamii.


"Katika Mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya vijana 2,685 walipatiwa mafunzo haya katika Mikoa ya Dodoma, Kagera, Manyara, Kigoma, Shinyanga, Mwanza na Arusha,"amesema.

No comments:

Post a Comment