WIZARA YA FEDHA YAKUSANYA ASILIMIA 82 YA FEDHA MWAKA 2023/2024 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 4, 2024

WIZARA YA FEDHA YAKUSANYA ASILIMIA 82 YA FEDHA MWAKA 2023/2024


Na Okuly Julius Dodoma

Wizara ya Fedha ilikadiriwa
kukusanya shilingi trilioni 39.79, kati ya makadirio yote ya Serikali ya kukusanya jumla ya shilingi trilioni 44.39 kwa mwaka 2023/24.

Kati ya kiasi hicho, Fungu 21
lilitarajiwa kutafuta na kukusanya jumla ya shilingi trilioni 39.74 ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania
ilikadiriwa kukusanya shilingi trilioni 26.73, Idara ya Fedha za Nje shilingi trilioni 5.47 na Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali shilingi trilioni 7.54; Fungu 23 lilikadiriwa kukusanya shilingi bilioni 60; na Fungu 50 shilingi milioni 300.


Amabapo hadi Aprili 2024, wizara imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 32.49,.sawa na ufanisi wa asilimia 82 ya lengo la mwaka.


Kati ya kiasi hicho, Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya jumla ya shilingi trilioni 21.31, Idara ya Fedha za Nje shilingi trilioni 4.92, Idara ya Usimamizi
wa Deni la Serikali shilingi trilioni 6.18 na maduhuli kupitia Fungu 23 shilingi bilioni 79.23 na Fungu 50
shilingi milioni 950.

No comments:

Post a Comment