WATAFITI WASHAURI WANANCHI KUJIUNGA BIMA YA UHIFADHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 13, 2024

WATAFITI WASHAURI WANANCHI KUJIUNGA BIMA YA UHIFADHI



Na Okuly Julius, Dodoma


WATAFITI wa Uhifadhi na Mazingira kutoka Vyuo Vikuu vya Ndani na Nje ya Nchi wameshauri Serikali kufanyia kazi matokeo ya utafiti wa mahusiano ya Simba na Binadamu kwa kuanzisha Bima ya Uhifadhi ili kufidia hasara inayosababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu wakiwemo Tembo wanaovamia mashamba na makazi ya wananchi.


Akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa utafiti wa mazingira na Ekolojia unauhusianisha siasa na Uongozi , Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt. Mathew Mabele amesema kulingana na Utafiti wa mahusiano kati ya Simba na Binadamu uliofanywa na watafiti kutoka chuo hicho, kuanzia 2018 hadi 2022, unonesha asilimia 72 ya wananchi waishio jirani na hifadhi ya taifa ya Ruaha waliohojiwa walieleza kuwa tayari kuchangia Bima ya Uhifadhi.

" wenzetu Kenya wameshaanza kulipia Bima ya Uhifadhi na wananchi wamefurahia kwani inawasaidia pale wanapopata madhara yanayosababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu wakiwemo Tembo wanaovamia mashamba na makazi ya wananchi," ameeleza Dkt. Mabele



Kwa upande wake Mhadhiri Idara ya Jiografia na Mazingira kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt. Whlem Kiwango, amesema mkutano huo wa kimataifa wa tafiti umefanyika vyuo vikuu vitatu kutoka katika nchi Tatu tofauti ambapo ni vyuo vikuu vya Lund- Sweden, Lima-Peru na UDOM nchini Tanzania na tafiti zilizowasilishwa zimejikita katika sehemu kuu tatu ambazo ni utatuzi wa changamoto za kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, kutoweka kwa bionuawai na taka.


Ambapo, sehemu nyingine ya Utafiti huo ni kuhusu Jamii za Kiasili ambapo hapa nchini watafiti wameangazia jamii ya Wahadzabe wakibainisha kuwa ni miongoni mwa zinazokabiliwa na changamoto za mazingira hivyo kuwa hatarini kutoweka.


Msisitizo wa watafiti hawa ni kuwa serikali, Mashirika yasiyo ya Serikali na washirika wa maendeleo katika mataifa yote wahamashike kutumia matokeo ya tafiti ili kulinda uhifadhi.






No comments:

Post a Comment