OR-TAMISEMI
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassima Majaliwa, mazindua rasmi Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) pamoja na ile ya shule za Sekondari (UMISSETA) ambayo inayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu amezindua mashindano hayo katika Uwanja wa ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora, huku akisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt. Samia suluhu Hassan inaamini kwenye uwekezaji katika michezo ya wanafunzi wa shule ya Msingi na sekondari Nchini.
“Mhe.Rais Dkt.Samia suluhu Hassana anawapenda sana na anayo matumaini makubwa kuwa, michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA itaendelea kuwa dirisha la matumaini katika kuimarisha na kuinua viwango vya michezo hapa nchini kwa kutoa wanamichezo bora hivyo anawatakia kila la kheri katika michezo hii”
“Serikali inaamini katika uwekezaji kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, uwekezaji huu unachagia kwa asilimia kubwa maandalizi ya mchezaji mwenye umahiri ambao pia wataweza kufanya vizuri ndani na nje ya nchi na hii ndio maana hasa ya uwepo wa michezo hii katika ngazi ya Taifa” amesema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameeleza umihimu wa mashindano hayo katika kukuza michezo na vipaji nchini, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji michezoni ambao utalisaidia taifa katika siku zijazo.
Mhe. Mchengerwa amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya mwaka huu kutafanyika uzinduzi wa timu timu za Taifa watakaotokana na michezo ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024, ambao unalenga kuandaa wachezaji watakaotumikia Taifa katika siku za mbeleni.
“Hivi karibuni baada ya Mashindano haya, tutazindua timu za taifa za vijana hawa, ni jukumu la vijana kuhakikisha wanatumia weledi wao wote katika mashindano haya tuone ujuzi wao wote kuhakikisha kwamba mionmgoni mwao wapatikane wachezaji watakaounda timu hizi za Taifa ambazo tutazitaja baada ya mashindano haya” amesema Mchengerwa
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA 2024 yananaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, yakiwa na kauli Mbiu isemayo “Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu, michezo na Sanaa, Hima Mtanzania shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024”
No comments:
Post a Comment