FAMILIA YAMTAKA BIDEN ABAKI KATIKA MBIO ZA KUINGIA IKULU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 1, 2024

FAMILIA YAMTAKA BIDEN ABAKI KATIKA MBIO ZA KUINGIA IKULU.



Familia ya Rais wa chama cha Democratic Joe Biden imemtaka kupuuza wito wa kujiuzulu baada ya mjadala dhidi ya Donald Trump wa chama cha Republican. 


Jumapili alikaa na jamaa zake ambao walimtia moyo kuendelea kupigana, kulingana na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News. 


Wasiwasi umekumba sehemu fulani za chama chake kufuatia kufanya vibaya kwenye mdahalo huko Atlanta. Kura za maoni tangu wakati huo zinaonesha wasiwasi kuhusu umri wake.


Kura ya maoni ya CBS News/YouGov iliyotolewa Jumapili ilionesha kuwa 72% ya wapiga kura wa Democratic waliojiandikisha wanaamini kuwa rais hana afya nzuri ya akili ya kuhudumu nafasi ya urais.


Karibu nusu walisema anapaswa kujiondoa. Lakini ujumbe kutoka kwa timu yake ya kampeni na familia yake ni kwamba anasalia kuwa tumaini bora la chama kumshinda Trump. 


Mkutano wa familia, Camp David huko Maryland ulikuwa umeratibiwa hapo awali kama upigaji picha na mpiga picha mashuhuri Annie Leibovitz. 


Mkewe Bw Biden Jill, watoto wake na wajukuu walikuwa miongoni mwa waliohudhuria. 


Kutiwa moyo kwa familia hiyo kusalia kwenye mbio hizo kuliripotiwa kwanza na New York Times na baadaye kuthibitishwa na CBS News.

No comments:

Post a Comment