IDADI TA WALIOFARIKI KATIKA MAANDAMANO YA KENYA YAFIKIA 39 - TUME YA HAKI ZA KIBINADAMU YA KENYA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 2, 2024

IDADI TA WALIOFARIKI KATIKA MAANDAMANO YA KENYA YAFIKIA 39 - TUME YA HAKI ZA KIBINADAMU YA KENYA.



Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu nchini Kenya (KNCHR) imesema idadi ya waliofariki dunia imefikia 39 huku 361 wakijeruhiwa tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga mswada wa Fedha 2024 kote nchini humo. 

‘’Uchunguzi wa maiti kwa wengi wa waathiriwa bado haujafanywa,’’ Tume hiyo imesema. 


Tume ya KNCHR pia imesema kumekuwa na taarifa za watu kutekwa nyara na kukamatwa kiholela. 


Kuna visa ‘’32 za upotevu wa kulazimishwa au kupotea bila kukusudia na 627 za kukamatwa kwa waandamanaji,’’kulingana na Tume hiyo.


Baadhi ya watu wanasemekana kuwa mafichoni kutokana na vitisho dhidi ya maisha yao na watu wasiojulikana.


Katika ripoti yake, Tume hiyo imeendelea kushtumu utumiaji wa nguvu kipita kiasi dhidi ya waandamanaji na wengineo kama wafanyakazi wa afya, waandishi wa habari na kwenye maeneo salama kama vile makanisa na vituo vya dharura vya matibabu. 


Serikali haijathibitisha idadi hiyo lakini Rais William Ruto siku ya Jumapili, Juni 30, wakati wa kikao na wanahabari, alisema kufikia wakati huo waliofariki walikuwa 19.


Rais aliongeza kuwa maafisa wa polisi walitekeleza majukumu yao kwa njia huru wakati wa maandamano hayo.


Kulingana na vyombo vya habari vya ndani tayari maandamano yameanza katika maeneo kama vile Mombasa licha ya Rais Ruto kutangaza Jumatano iliyopita kwamba hatatia saini Mswada tata wa Fedha kuwa sheria.

No comments:

Post a Comment