HALI YA WASIWASI YAENDELEA KUSHUHUDIWA KATI YA SOMALIA NA ETHIOPIA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 2, 2024

HALI YA WASIWASI YAENDELEA KUSHUHUDIWA KATI YA SOMALIA NA ETHIOPIA.

 


Rais wa Somalia Hassan Sheik Mohamud amesema hakuna dalili za Ethiopia kujiondoa kwenye makubaliano ya bandari yenye utata ambayo yalizua mvutano kati ya nchi hizo mbili. 

Rais alikuwa akizungumza baada ya wajumbe kutoka nchi hizo mbili za Pembe ya Afrika- wakiongozwa na mawaziri wao wa mambo ya nje- kufanya mazungumzo nchini Uturuki kwa lengo la kurekebisha uhusiano wao.

Makubaliano yasiyo ya lazima ambayo ndio msingi wa mvutano wao yaliotiwa saini mwezi Januari kati ya Addis Ababa na jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland- yamefungua njia kwa Ethiopia isiyo na bandari kuwa na kilomita 20 za ukanda wa pwani. 

Ethiopia kwa upande wake inaweza kutambua Somaliland inayochukuliwa na Mogadishu kama sehemu ya eneo lake kama nchi huru.

Somalia inaona makubaliano hayo kama uchokozi.

Hakuna mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mazungumzo hayo ambayo yalikuwa ya kwanza tangu mpango huo kutangazwa. 

Lakini ukweli kwamba yalifanyika unaonekana kama maendeleo na nchi hizo mbili zimekubaliana kukutana tena mnamo mwezi Septemba.

Kulingana na Sheik Mohammed mazungumzo hayo yaliombwa na Ethiopia, lakini majadiliano ya moja kwa moja hayakufanyika.


No comments:

Post a Comment