Polisi wa Kenya wamefyatua gesi ya kutoa machozi katika mji mkuu Nairobi kutawanya maandamano ya kuipinga serikali.
Katikati ya jiji biashara nyingi zimefungwa.
Waandamanaji pia wameingia katika mitaa ya miji mingine ikiwemo Mombasa na Kisumu.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema tangu maandamano ya kupinga muswada wenye utata wa fedha kuanza wiki mbili zilizopita watu 39 wameuawa na vikosi vya usalama.
Rais William Ruto tangu wakati huo ametupilia mbali mapendekezo ya nyongeza ya ushuru, lakini maandamano yamebadilika na kuwa wito wa kujiuzulu na hasira juu ya ukatili wa polisi.
No comments:
Post a Comment