TAKRIBAN WATU 24 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA URUSI KATIKA MIJI YA UKRAINE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 8, 2024

TAKRIBAN WATU 24 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA URUSI KATIKA MIJI YA UKRAINE.

 


Takriban watu 20 wameuawa baada ya Urusi kufanya shambulizi kubwa la kombora dhidi ya miji kote Ukraine, kulingana na maafisa.


Katika mji mkuu, Kyiv, takriban watu saba waliuawa katika shambulio la nadra la mchana. 


Meya wa jiji hilo alisema hospitali ya watoto imeshambuliwa kwa makombora na wagonjwa wanahamishwa.


Mkuu wa utawala wa kijeshi katika mji wa kati wa Ukraine wa Kryvyi Rih amesema takriban watu 10 wameuawa huko, huku watatu wakiuawa katika mji wa mashariki wa Pokrovsk.


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye anazuru Poland, alisema kuwa Urusi imefyatua takriban makombora 40 kulenga shabaha kote nchini.


Bw Zelensky, ambaye anatazamiwa kusafiri hadi Marekani kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Nato wa wiki hii mjini Washington, alisema Urusi "imeishambulia kwa kiasi kikubwa" Ukraine.


"Miji tofauti: Kyiv, Dnipro, Kryvyi Rih, Sloviansk, Kramatorsk. Zaidi ya makombora 40 ya aina mbalimbali. Majengo ya makazi, miundombinu na hospitali ya watoto yaliharibiwa, "alisema.


Moshi mwingi ulionekana katika mji mkuu wa Kyiv, huku video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha uharibifu ndani na nje ya hospitali ya watoto ya Okhmadyt. 


Haijabainika iwapo mtu yeyote ndani alijeruhiwa.


Lakini Bw Zelensky alisema katika ujumbe wa mtandao wa kijamii kwamba watu walinaswa chini ya vifusi vya hospitali hiyo. 


Aliongeza kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa katika hospitali ya Okhmadyt haijulikani.


Vitaliy Klitschko, meya wa Kyiv, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba shambulio hilo lilikuwa baya zaidi katika mji mkuu huo tangu kuanza kwa vita.


Kwingineko, Oleksandr Vilkul, mkuu wa utawala wa kijeshi huko Kryvy Rih, alichapisha kwenye programu ya Telegram ujumbe kwamba watu wasiopungua 10 waliuawa na 31 kujeruhiwa kufuatia shambulio la mji huo. 


Kati ya hao, alisema 10 walijeruhiwa vibaya.


Kryvy Rih ni mji alikozaliwa Bw Zelensky na umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na Urusi tangu ilipoanzisha uvamizi wake huko Ukraine mnamo Februari 2022.

No comments:

Post a Comment