JESHI LA UKRAINE LABORESHA UJUZI WA KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI- ISW. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 8, 2024

JESHI LA UKRAINE LABORESHA UJUZI WA KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI- ISW.


Waendeshaji wa ndege zisizo na rubani za Ukraine wanaboresha uwezo wao wa kunasa ndege zisizo na rubani za Urusi za masafa marefu, Taasisi ya Amerika ya Utafiti wa Vita (ISW) inaandika katika ripoti ya kawaida ya kila siku.


Kulingana na wataalamu hao, uvumbuzi huo wa kiteknolojia unaweza kuviruhusu vikosi vya Ukraine kupunguza mzigo kwenye mifumo ya ulinzi wa anga ikiwa itatumika kwa ufanisi kote nchini.


Picha zilizotolewa mnamo tarehe 1 Juni zinaonyesha vikosi vya Ukraine vikitumia ndege zisizo na rubani za aina ya FPV kushambulia ndege isiyo na rubani ya Urusi ya upelelezi aina ya Zala na ndege nyingine isiyo na rubani ya masafa ya kati aina ya Orlan-10.


Mwishoni mwa mwezi Juni, jeshi la Ukraine pia lilichapisha picha za ndege isiyo na rubani yaUkraine ikinasa ile ya Urusi aina ya Lancet UAV angani katika iliyokua ikielekea Kharkov.


Vikosi vyote vya Ukraine na Urusi vinaonekana kuboresha uwezo wao wa ndege zisizo na rubani katika kiwango cha mbinu, lakini ISW bado haijapata ushahidi wa vikosi vya Urusi vinavyotumia ndege zisizo na rubani za FPV kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya droni za kamikaze au UAV za masafa marefu za upelelezi.

No comments:

Post a Comment