Na Jasmine shamwepu,Dodoma.
Mkurugenzi wa elimu kwa umma kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru )Joseph Mwaiselo
amesema ili kupambana na rushwa ni muhimu Wanasiasa wanapaswa kuwa na misingi ya uwazi,uwajibikaji,uaminifu katika kutumia fedha kipindi Cha uchaguzi Kwa wagombea au vyama vya siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Jukwaa la uwajibikaji la vijana (YA IF)amesema Kwa mujibu wa Sheria ya gharama za uchaguzi fedha hizo zinahitaji kuwa na misingi ya uwajibikaji na uwazi ili kupambana na rushwa.
"Vijana wanapopata elimu hii ya msingi katika nchi yetu ya Tanzania katika kuelekea uchaguzi huru na haki itasaidia namna ya kutumia fedha hizo katika chaguzi,amesema Kasongwa
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la vijana la uwajibikaji taifa Antipas Pamba amesema wanataka kuona vijana wakishiriki vyema katika masuala ya uwajibikaji hasa katika rasilimali fedha ili kujengewa uwezo katika taasisi.
Pamba amesema masuala ya rasilimali fedha ni maeneo ambayo wanataka watu washiriki ikiwa wajibu wa Baraza na vlabu mbalimbali vyuoni ili kuhakikisha kizazi Cha vijana kinajengwa kitakachosaidia dhamira njema ya viongozi wa juu ya nchi.
"Tunajifunza mambo mbalimbali ikiwemo michakato ya bejeti ya taifa na namna kijana au mwananchi wa kawaida anavyoweza kuingia pale kushiriki kwani mambo Yale yanaanza katika ngazi ya chini ya Serikali za mitaa"Amesema Mwenyekiti wa vijana.
Aidha amesema uwajibikaji una mambo mengi ikiwemo ukusanyaji wa Kodi na masuala ya rushwa yaliletwa jinsi ya kudhibiti mianya ya rushwa kwenye sekata za umma kupitia teknolojia.
Antipas amesema mwaka huu wamekuwa wakiangalia dhana kubwa ya uwajibikaji na uwazi unaoathiri masula ya uchaguzi ikiwa Nchi inaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.
Naye Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na mshindi wa mashindano ya insha Rosemary Chondi amesema kupitia mada ya uwajibikaji ushindi alioupata Suala kubwa
la kuzingatia ni pamoja na kuelezea jinsi uwazi na uwajibikaji vinavyochukua nafasi kubwa katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura.
"Maeneo mengi ya Tanzania wananchi wengi wanakuta wakijiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura lakini hawajitokezi kwenda kupiga kura ikiwa sababu kukosa imani na watu waliowekwa katika misingi ya kusimamia uchaguzi"Amesema Chondi
No comments:
Post a Comment