Na; Mwandishi Wetu – Arusha
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka viongozi wa Ofisi hiyo kufanya kazi katika ubora na ueledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwahudumia Watanzania.
Ameyasema hayo mapema leo tarehe 1 Agosti 2024 Jijini Arusha alipohitimisha kikao za mazingativu (Retreat) kilichohusisha viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Menejimenti, Watumishi na Taasisi zilicho chini ya Ofisi hiyo.
Dkt. Yonazi alisema kuwa ana imani kubwa kwa watumishi na viongozi wa Ofisi hiyo kuwa watakuwa ni watumishi wenye thamani na utulivu na wenye nia ya kuwatumikia Watanzania kwa weledi na moyo Thabiti.
“Sisi hapa wengi ni viongozi, watu wa chini yetu ndo wametuwezesha kuwa viongozi hivyo tumesiweke mazingira magumu kwa waliyopo chini yetu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.” Alibainisha Dkt. Yonazi
Aidha, Dkt. Yonazi aliwashukuru Viongozi wa juu wa Ofisi hiyo kwa Maandaliz mazuri ya kikao hicho cha siku tatu cha mazingativu kilichokuwa na lengo la kuendeleza mafunzo kazini kuwaleta watumishi na viongozi pamoja kwa ajili ya kujifunza na kuwa na mbinu ambazo zitaweza kuboresha utendaji wa shughuli za kila siku za Ofisi.
Awali akizunguza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Mipango na Bajeti kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Eleuter Kihwele amesema mafunzo hayo yalishafanyika mwaka 2023 na yamesaidia sana katika kuboresha utendaji kazi na kusaidia kuimarisha umoja kwa kuwaleta pamoja watumishi wote.
Aliongezea kuwa utendaji wa pamoja katika maana ya viongozi na watumishi kukaa pamoja kujadili pamoja namna ya kuleta Tija katika uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa shughuli za Serikali unachochea ufanisi kazini na kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.
Xxxxx MWISHO xxxxxx
CAPTIONS
Picha No 1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akihitimisha kikao cha Mazingativu (Retreat) kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake, Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.
Picha no 2
Baadhi ya Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakiwa katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.
Picha no.3
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge an Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa akitoa neno la shukrani katika kikao cha Mazingativu (Retreat) kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya hiyo, watumishi na Taasisi zilizo chini yake, Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.
Picha no 4
Muwezeshaji wa mada inayohusu staili ya maisha na Nidhamu ya vyakula Dkt. Fredrik Lazaro Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili akitoa mada katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.
Picha no 5
Sehemu ya Washiriki katika kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.
Picha no 6
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akigawa vyeti kwa viongozi wakati wa kikao cha Mazingativu kinachohusisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) watumishi na Taasisi zilizo chini yake, kilichomalizika Jijini Arusha Tarehe 1 Agosti 2024.
No comments:
Post a Comment